SURA YA 114
SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI

[SUBSIDIARY LEGISLATION]

INDEX TO SUBSIDIARY LEGISLATION

   KANUNI

      Kanuni za Ardhi ya Vijiji

ORODHA YA KANUNI

KANUNI ZA ARDHI YA VIJIJI

   Kanuni

Jina

SEHEMU YA I
MAMBO YA AWALI

   1.   Jina.

   2.   Ufafanuzi.

SEHEMU YA II
USIMAMIZI NA UTAWALA

   3.   Taarifa.

   4.   Amri.

   5.   Wito.

   6.   Viapo.

   7.   Utaratibu wakati taasisi za kijiji zinasikiliza mashauri.

SEHEMU YA III
FIDIA

   8.   Nani aweza kudai fidia.

   9.   Misingi ya ukadiriaji.

   10.   Bei katika soko.

   11.   Mthamini aliyehitimu.

   12.   Mthamini Mkuu.

   13.   Fidia.

   14.   Posho ya upangaji.

   15.   Kupoteza faida.

   16.   Posho ya usumbufu.

   17.   Posho ya usafiri.

   18.   Ardhi isiyokaliwa.

   19.   Riba.

   20.   Kupewa taarifa ya kudai fidia.

   21.   Madai ya fidia.

   22.   Msaada wa kutayarisha madai ya fidia.

   23.   Kukubali madai ya fidia.

   24.   Usuluhishi kuhusu madai ya fidia.

   25.   Aina za fidia.

SEHEMU YA IV
USIMAMIZI WA PAMOJA WA ARDHI YA KIJIJI

   26.   Pendekezo la usimamizi wa pamoja wa ardhi ya kijiji.

   27.   Kupigia kura pendekezo la usimamizi wa pamoja wa ardhi ya kijiji.

   28.   Kukataliwa kwa pendekezo la usimamizi wa pamoja wa ardhi ya kijiji.

   29.   Uteuzi wa Kamati ya Pamoja.

   30.   Tafakari ya rasimu ya Mpango wa Usimamizi wa Pamoja.

   31.   Marekebisho ya rasimu ya Mpango wa Usimamizi wa Pamoja.

   32.   Makubaliano ya Mpango wa Usimamizi wa Pamoja.

   33.   Kamati ya Pamoja inawajibika kwa uendeshaji wa usimamizi wa pamoja.

   34.   Vipengele vinavyoelekeza uendeshaji wa Kamati ya Pamoja.

   35.   Yaliyomo katika Mpango wa Usimamizi wa Pamoja.

SEHEMU YA V
DAFTARI LA ARDHI YA KIJIJI

   36.   Sehemu za Daftari.

   37.   Cheti cha Ardhi ya Kijiji.

   38.   Daftari la Hati.

   39.   Daftari Bayana la Kutahadharisha.

   40.   Watu wanaostahili kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya usajili.

   41.   Taratibu za usajili.

   42.   Utoaji wa namba na hifadhi ya nyaraka zilizosajiliwa.

   43.   Kumbukumbu kimaandishi iliyoambatishwa na waraka uliosajiliwa.

   44.   Kitabu cha muhtasari.

   45.   Shughuli za miliki za ardhi.

   46.   Mwenye haki kutaarifiwa.

   47.   Jukumu la Afisa kwenye shughuli za ardhi.

   48.   Kipaumbele.

   49.   Afisa aweza kukataa kusajili nyaraka.

   50.   Uwezo wa Afisa kusahihisha makosa.

   51.   Usajili hautaondoa kasoro au kuhalalisha.

   52.   Daftari laweza kukaguliwa na nakala kupatikana.

   53.   Nyaraka mbadala ya iliyosajiliwa.

   54.   Nakala ya waraka uliyosajiliwa.

   55.   Kupatikana waraka asili uliyosajiliwa.

   56.   Kupatikana nakala ya waraka uliosajiliwa.

   57.   Nakala ya waraka potevu uliyosajiliwa.

   58.   Nakala iliyothibitishwa ya waraka uliyosajiliwa kukubalika katika kesi za madai.

   59.   Matumizi ya nakala iliyothibitishwa ya waraka uliyosajiliwa katika kesi za madai.

   60.   Muda wa Masjala kuwa wazi.

SEHEMU YA VI
UAMUZI WA MASLAHI NA MIPAKA KATIKA ARDHI

   61.   Taarifa kwa pande zinazohusika.

   62.   Kuweka mipaka.

   63.   Uthibitisho wa mipaka.

   64.   Kusafisha na kuweka alama kwenye mipaka.

   65.   Kutunza mipaka.

   66.   Kipimo cha upimaji.

   67.   Matayarisho ya mchoro.

   68.   Taratibu za upimaji.

   69.   Kuweka kumbukumbu ya haki za njia.

   70.   Mgao wa mchoro.

   71.   Kumbukumbu za uamuzi wa maslahi na mipaka katika ardhi.

   72.   Taarifa ya upimaji wa ardhi inayomilikiwa kwa hakimiliki ya kimila iliyosajiliwa.

   73.   Namba ya Utambulisho wa Kipande cha Ardhi.

   74.   Mgawanyo.

SEHEMU YA VII
MENGINEYO

   75.   Waziri aweza kuweka viwango vya juu vya kumiliki ardhi.

   76.   Taratibu za idhini ya viwango vya juu vya kumiliki ardhi.

   77.   Misingi ya jumla ya usuluhishi.

   78.   Maandalizi ya nyaraka.

   79.   Fomu zitakazotumika kuhusiana na Sheria na Kanuni hizi.

   80.   Mabadiliko ya fomu.

   81.   Ada.

   82.   Faini.

   83.   Ushuhuda wa Kusaini Nyaraka.

JEDWALI LA KWANZA
FOMU

SEHEMU YA I
USIMAMIZI NA UTAWALA

   Fomu Na. 1    Amri ya kuitwa kwenye Kamati ya Uamuzi ya Kijiji.

   Fomu Na. 2   Amri ya kuwasilisha nyaraka mbele ya Kamati ya Uamuzi ya Kijiji.

   Fomu Na. 3   Wito wa kuhudhuria kusikilizwa mbele ya Kamati ya Uamuzi wa Kijiji.

   Fomu Na. 4   Wito wa kuhudhuria kusikilizwa mbele ya Baraza la Ardhi la Kijiji.

   Fomu Na. 5   Kiapo cha shahidi.

   Fomu Na. 6   Taarifa ya kusudio la kutangaza ardhi yenye madhara.

   Fomu Na. 7   Taarifa ya kuitangaza ardhi yenye madhara.

   Fomu Na. 8   Taarifa ya kusudio la kuhawilisha Ardhi ya Kijiji kuwa ardhi ya kawaida au ardhi ya hifadhi.

   Fomu Na. 9   Taarifa ya kuhawilisha Ardhi ya kijiji.

   Fomu Na. 10   Tamko la mgongano wa maslahi.

SEHEMU YA II
FIDIA

   Fomu Na. 11   Taarifa kwa Halmashauri ya Kijiji kudai fidia.

   Fomu Na. 12   Ombi la Halmashauri ya Kijiji kulipwa fidia.

   Fomu Na. 13   Kibali cha fidia.

   Fomu Na. 14   Taarifa kwa mkazi kudai fidia.

   Fomu Na. 15   Ombi la mkazi kudai fidia.

SEHEMU YA III
DAFTARI LA ARDHI YA KIJIJI

   Fomu Na. 16   Cheti cha Ardhi ya Kijiji.

   Fomu Na. 17   Kitabu cha Muhtasari.

SEHEMU YA IV
HAKIMILIKI ZA KIMILA

   Fomu Na. 18   Ombi la hakimiliki ya Kimila.

   Fomu Na. 19   Ahadi ya toleo la hakimiliki ya kimila.

   Fomu Na. 20   Kukubali ahadi ya Toleo la Hakimiliki ya Kimila.

   Fomu Na. 21   Cheti cha Hakimiliki ya Kimila.

   Fomu Na. 22   Ombi la nakala ya Cheti cha Hakimiliki ya Kimila.

   Fomu Na. 23   Taarifa ya kulipa kodi.

   Fomu Na. 24   Taarifa ya Uhakilishaji wa Hakimiliki ya Kimila.

   Fomu Na. 25   Kukubaliwa Kukataliwa kwa uhakilishaji wa hakimiliki ya kimila.

   Fomu Na. 26   Ombi la kibali cha kutoa hakimiliki isiyo asili.

   Fomu Na. 27   Cheti cha kibali cha hakimiliki isiyo asili upangishaji leseni haki ya matumizi.

   Fomu Na. 28   Ombi la kutoa hakimiliki isiyo asili kwenye kijiji.

   Fomu Na. 29   Kutolewa kwa hakimiliki isiyo isili kwenye ardhi ya kijiji.

   Fomu Na. 30   Kurejesha hakimiliki ya kimila.

   Fomu Na. 31   Barua ya onyo.

   Fomu Na. 32   Kibali kwa hatua ya Halmashauri ya Kijiji.

   Fomu Na. 33   Ilani ya kujieleza.

   Fomu Na. 34   Taarifa ya kulipa taini.

   Fomu Na. 35   Taarifa ya kurekebisha ukiukaji wa masharti.

   Fomu Na. 36   Amri ya Usimamizi.

   Fomu Na. 37   Ombi la idhini ya uhakilishaji kwa muda.

   Fomu Na. 38   Taarifa ya uhakilishaji kwa muda wa hakimiliki ya kimila.

   Fomu Na. 39   Agizo la masharti ya uhakilishaji kwa muda.

   Fomu Na. 40   Leseni ya Makazi.

   Fomu Na. 41   Taarifa ya kubaini utelekezaji ardhi.

   Fomu Na. 42   Tamko la utelekezaji ardhi.

SEHEMU YA V
UAMUZI KUHUSU MASLAHI NA MIPAKA KATIKA ARDHI

   Fomu Na. 43   Ombi la kibali kuhusu shughuli ya ardhi mavozidi kiwango cha juu cha ardhi kwa kijiji.

   Fomu Na. 44   Ombi la Maamuzi kwa Eneo Maalumu.

   Fomu Na. 45   Pendekezo la kutumia Uamuzi Ngazi ya Kijiji.

   Fomu Na. 46   Taarifa ya Kamati ya Uamuzi ya Kijiji kusikiliza masuala ya ardhi.

   Fomu Na. 47   Uthibitisho wa mipaka.

   Fomu Na. 48   Taarifa ya upimaji wa mipaka ya hakimiliki ya kimila.

   Fomu Na. 49   Kugawanya hakimiliki ya kimila.

   Fomu Na. 50   Kumbukumbu ya uamuzi wa maslahi na mipaka ya ardhi.

JEDWALI LA PILI
ADA

JEDWALI LA TATU
FAINI

KANUNI ZA ARDHI YA VIJIJI

(Zimetungwa chini ya fungu la 65)

G.N. No. 201 of 2002

SEHEMU YA I
MAMBO YA AWALI

1.   Jina

   Kanuni hizi ziitwe Kanuni za Ardhi ya Vijiji, 2002.

2.   Ufafanuzi

   Katika Kanuni hizi, isipokuwa tu pale ambapo maelezo yanahitaji vinginevyo:–

   "Afisa" maana yake ni Afisa Mtendaji wa kijiji;

   "Afisa Ardhi wa Wilaya" maana yake ni Afisa Mteule aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Ardhi;

   "Afisa Mtendaji wa Kijiji" maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji kwa mujibu wa sheria husika;

   "Baraza" maana yake ni Baraza la Ardhi la Kijiji lililoundwa chini ya fungu la 60 la Sheria;

   "Daftari la Ardhi ya Kijiji" maana yake ni daftari la ardhi ya kijiji linalotunzwa kwa mujibu wa fungu la 21 la Sheria;

   "daimiliki kwa nyaraka zilizowasilishwa" maana yake ni kuwasilisha waraka wowote uliotajwa katika aya za (ii), (iv) na (v) za ibara ya (b) ya kifungu cha (6) cha fungu la 112 la Sheria ya Ardhi;

   "hakimiliki isiyo asili" maana yake ni kama ilivyofafanuliwa na Sheria;

   "hakimiliki ya kimila" maana yake ni kama ilivyofafanuliwa na Sheria;

   "Kamati" maana yake ni Kamati ya Uamuzi ya Kijiji iliyoundwa chini ya fungu la 53 la Sheria, na ni pamoja na Afisa Mwamuzi anayetumia mamlaka yake chini ya Fungu la 56 la Sheria;

   "Mahakama" maana yake ni kama ilivyofafanuliwa na Sheria;

   "Mamlaka ya Serikali ya Mtaa" maana yake ni kama ilivyofafanuliwa katika fungu la 2 la Sheria;

   "Masjala ya Ardhi ya Wilaya" maana yake ni Masjala ya Ardhi ya Wilaya iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Usajili;

   "maslahi katika shauri" maana yake ni maslahi, kifedha au vinginevyo, yanayoweza kupunguza ubora wa wajibu wa mtu katika kusikiliza na kuamua jambo lolote, na ni pamoja na maslahi ya ndugu wa damu au kutokana na uhusiano wa ndoa;

   "mkazi" maana yake ni mmiliki wa hakimiliki ya kimila;

   "Mthamini Aliyehitimu" maana yake ni kama ilivyofafanuliwa kwenye fungu la 2 la Sheria ya Ardhi *;

   "rehani isiyo rasmi" maana yake ni rehani kama ilivyofafanuliwa kwenye ibara (a) ya kifungu cha (6) cha fungu la 112 la Sheria ya Ardhi;

   "Serikali" maana yake ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

   "Sheria" maana yake ni Sheria ya Ardhi ya Vijiji *;

   "taasisi ya kijiji" maana yake ni Halmashauri ya Kijiji, Kamati ya Halmashauri ya Kijiji, Kamati ya uamuzi Ngazi ya Kijiji na Afisa Mwamuzi anayetekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa fungu la 56 la Sheria.

   "utaratibu wa usimamizi wa pamoja" maana yake ni utaratibu wa usimamizi wa ardhi ya kijiji unaoweza kuwekwa kwa mujibu wa fungu la 8 la Sheria;

   "waraka uliosajiliwa" maana yake ni cheti cha hakimiliki ya kimila au hakimiliki isiyo asili kinachotolewa kwa mujibu wa sehemu ya IV ya Sheria, kilichomo kwenye Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi,

SEHEMU YA II
USIMAMIZI WA UTAWALA

3.   Taarifa

   Taarifa ya kusikilizwa kwa shauri lolote na taasisi ya kijiji kwa mujibu wa Kanuni hizi itatolewa kama ilivyo kwenye Jedwali la Kwanza.

4.   Amri

   Amri mayomtaka mtu ahudhurie kikao au awasilishe waraka mbele ya taasisi ya kijiji itaandikwa kwenye fomu maalum zilizoonyeshwa katika Jedwali la Kwanza.

5.   Wito

   (1) Wito unaotolewa na Mwenyekiti wa Kamati, au Afisa Mwamuzi anayetumia mamlaka chini ya fungu la 56 la Sheria, kwa mtu anayetakiwa kuhudhuria kwa mujibu wa fungu la 54 la Sheria ya Ardhi ya Vijiji lazima umpe taarifa ya siku zisizopungua 14 kabla ya tarehe anapotakiwa kuhudhuria kusikilizwa shauri.

   (2) Wito kwa mujibu wa kanuni hii utatolewa kama ulivyoonyeshwa kwenye Jedwali la Kwanza.

6.   Viapo

   Kiapo anachoweza kuapisha Mwenyekiti wa Kamati au Afisa Mwamuzi anayetumia mamlaka chini ya fungu la 56 la Sheria kinaweza kuwa kama kilivyoonyeshwa kwenye Jedwali la Kwanza.

7.   Utaratibu wakati taasisi za kijiji zinasikiliza mashauri

   Katika kusikiliza mashauri kwa mujibu wa Sheria au Kanuni Hizi, taasisi ya kijiji itawajibika kufuata taratibu za msingi ya haki za binadamu katika kuweka taratibu zake, na itawajibika–

   (a)   kuendesha usikilizaji wa mashauri hadharani na bila ya urasimu lakini kwa kufuata utaratibu, heshima na usawa kwa pande zote kufafanua wazi kwa wawakilishi wowote na taasisi hiyo ya kijiji itazingatia zaidi maswala ya msingi katika shauri lililoletwa na itatoa uamuzi juu ya haki bila kulazimika kuzingatia taratibu za kiufundi;

   (b)   kutomshirikisha katika kikao mjumbe wa taasisi ya kijiji mwenye maslahi katika shauri linalojadihwa, maslahi ambayo mjumbe huyo atawajibika kuyatangaza na kutohudhuria kikao wala kujihusisha kwa namna yoyote ile katika kusikiliza kama mjumbe wa taasisi ya kijiji;

   (c)   kabla ya kusikiliza shauri, kupanga na kutangaza saa ya mchana ya siku ambapo shauri litasikilizwa na katika kufanya hivyo itazingatia mazingira ya pande husika na mpangilio wa kawaida wa kazi katika eneo ambako shauri litasikilizwa;

   (d)   kuruhusu watu wote wanaotaka kutoa hoja mbele ya taasisi ya kijiji wafike mbele ya taasisi hiyo wao binafsi au kwa kuwakilishwa;

   (e)   kuruhusu mtu aliyeitwa shaurini atoe hoja yake kwanza na ndipo ahojiwe kuhusu jambo lolote kutokana na hoja yake, au aombwe na mjumbe aliyepo au mtu mwenye maslahi katika ardhi inayohusika katika shauri, kutoa taarifa za ziada kuhusu hoja yake;

   (f)   baada ya mtu aliyeitwa kutoa hoja yake, kuruhusu mtu yeyote aliye na madai juu ya ardhi husika atoe hoja yake na kuulizwa maswali na mjumbe yeyote aliyepo wa taasisi ya kijiji, na mtu yeyote aliyeitwa shaurini;

   (g)   Kuhusu mtu yeyote alete maelezo kwa mdomo au kimaandishi au kwa mdomo na pia kimaandishi;

   (h)   endapo taasisi ya kijiji itakusudia kuitisha ushahidi juu ya jambo au suala lolote, itawataarifu wahusika wa pande zote za shauri kuhusu uamuzi huo na kuwaruhusu kutoa maoni au kuuliza maswali kuhusu ushahidi huo;

   (i)   endapo taasisi ya kijiji itatembelea na kukagua ardhi mayohusika katika shauri linalosikilizwa, itaruhusu watu wanaodai kuwa na maslahi katika ardhi hiyo, waonyeshe alama za ardhi hiyo na watoe maelezo mengine kuhusu ardhi hiyo na maslahi yao katika ardhi hiyo;

   (j)   kwa kumtumia Mwenyekiti wa taasisi ya kijiji, au mjumbe, au afisa aliyeteuliwa na Mwenyekiti kwa ajili hiyo, kutunza kumbukumbu ya uendeshaji wa shauri lililosikilizwa, pamoja na kumbukumbu ya kutembelea ardhi yoyote wakati wa kusikiliza shauri;

   (k)   yaweza kukubali kama ushahidi kuhusu mipaka ya eneo la ardhi mayohusika katika shauri:

      (i)   tamko kuhusu mipaka litolewalo na mtu yeyote anayetambuliwa na jamii kama mtu mwaminifu na anayefahamu masuala ya ardhi katika kijiji;

      (ii)   aina rahisi au za kiasili za upimaji au uwekaji mipaka kwa kutumia alama asili na miti au majengo na vitu vinginevyo vinavyoonekana dhahiri;

      (iii)   shughuli za binadamu kwenye ardhi kama vile matumizi ya njia za miguu, mapito ya mifugo sehemu za kupata maji na uwekaji alama za mipaka katika ardhi;

      (iv)   ramani na michoro iliyochorwa kwa vipimo au bila vipimo rasmi mayoonyesha kwa rejea, jambo lolote lililotajwa katika aya ya (ii) au ya (iii) za ibara (K) mipaka ya eneo la ardhi;

   (l)   kuzingatia kwa umakini wa kipekee maslahi katika ardhi mayohusika na kusikiliza shauri linalowahusu wanawake, watoto na watu wasiojiweza, na kuhakikisha kwamba maslahi haya yanazingatiwa na kuwekewa kumbukumbu kikamilifu;

   (m)   katika kuamua kama mafaa kuahirisha usikilizaji wa shauri, yaweza kuahirisha shauri kwa lengo la kuzirahisishia pande husika kuondoa wao wenyewe tofauti walizonazo kuhusu maslahi ya kila upande katika ardhi na lazima kunukuu mapatano yoyote waliyoyafanya shauri litakapoanza tena kusikilizwa;

   (n)   kuzingatia uwezekano wakati wowote au baada ya kusikiliza jambo fulani, kutoa uamuzi wa awali kuhusu suala lolote, endapo itafanya uamuzi wa aina hii, iwaombe pande zote kutoa maoni yao juu ya uamuzi huo kwa mdomo au kwa maandishi;

   (o)   kujaribu kufikia maamuzi yote kwa muafaka lakini kama haitawekana, basi uamuzi wa walio wengi waweza kuchukuliwa na zinukuliwe sababu za uamuzi wa wengi na za wale wachache;

   (p)   katika kufikia uamuzi kama suala lolote limethibitishwa mbele ya taasisi ya kijiji, kuamua kama kumetolewa ushahidi wa kutosha yaani kama, uzito wa, hoja unaashiria zaidi kwamba jambo limethibitishwa kuliko kutothibitishwa;

   (q)   kuandaa taarifa itakayojumuisha–

      (i)   majina ya wajumbe wa taasisi ya kijiji iliyosikiliza shauri;

      (ii)   tarehe ya kusikiliza shauri;

      (iii)   majina ya watu wa pande husika;

      (iv)   muhtasari wa ushahidi wa pande zote na vya mashahidi wote;

      (v)   maamuzi kuhusu vipengele vyote vya shauri na madai pamoja na sababu za mapendekezo hayo;

      (vi)   mapendekezo kwa vipengele vyote wa shauri na madai pamoja na sababu za mapendekezo hayo;

   (r)   kusaini ripoti iliyotayarishwa kwa mujibu wa ibara (q).

SEHEMU YA III
FIDIA

8.   Nani aweza kudai fidia

   Wafuatao waweza kudai fidia kutokana na uhawilishaji wa ardhi ya kijiji kuwa ardhi ya kawaida au ardhi ya hifadhi chini ya fungu la 4 la Sheria, au kutokana na ardhi kutangazwa kuwa ardhi yenye madhara chini ya fungu la 6 la Sheria, na endapo Halmashauri ya Kijiji imeamua kwamba wakazi watatakiwa kuihama ardhi hiyo yenye madhara au sehemu ya ardhi hiyo:

   (a)   Halmashauri ya Kijiji kwa niaba ya wanakijiji waliopoteza ardhi ya pamoja ya kijiji, mali na mafao kutokana na ardhi ya pamoja ya kijiji;

   (b)   Mwanakijiji yeyote anayekalia ardhi iliyohawilishwa au ardhi yenye madhara chini ya hakimiliki ya kimila, bila kujali kama hakimiliki hiyo imesajiliwa au la.

9.   Misingi ya ukadiriaji

   Msingi wa kukadiria thamani ya ardhi yoyote na uboreshaji usiohamishika kwa ajili ya ulipaji wa fidia chini ya Sheria ni thamani ya ardhi hiyo katika soko.

10.   Bei katika soko

   Thamani ya ardhi katika soko inayoihusu ardhi yoyote na uboreshaji usiohamishika kutumia kigezo cha mlinganisho wa mauzo hali halisi ya karibuni ya ardhi au mali kama hiyo au kwa kutumia kigezo cha mapato au gharama ya kufidia endapo ardhi au mali ni ya aina yake ambayo haiwezi kuuzwa.

11.   Mthamini aliyehitimu

   Kila makadirio ya thamani ya ardhi na ya uboreshaji usiohamishika kwa malengo ya Sheria hii lazima yafanywe na mthamini aliyehitimu.

12.   Mthamini Mkuu

   Kila makadirio ya thamani ya ardhi na uboreshaji usiohamishika kwa ajili ya kulipa fidia itakayolipwa na Serikali Kuu au Serikali za Mitaa lazima yathibitishwe na Mthamini Mkuu wa Serikali au mwakilishi wake.

13.   Fidia

   Fidia kwa kupoteza maslahi yoyote kwenye ardhi itajumuisha thamani ya uboreshaji usiohamishika, posho ya usumbufu, posho ya usafiri, posho ya upangaji na kupoteza faida.

14.   Posho ua upangaji

   Kodi ya pango katika soko kwa jengo itakadiriwa na kuzidishwa mara miezi thelathini na sita (36) ili kupata posho ya upangaji itakayolipwa.

15.   Kupoteza faida

   Faida halisi kwa mwezi kwa biashara inayoendeshwa kwenye ardhi itakadiriwa na kuzidishwa mara miezi thelathini na sita (36) ili kufikia kiwango cha malipo ya faida inayopotea.

16.   Posho ya usumbufu

   Posho ya usumbufu itakadiriwa kwa kuzidisha thamani ya ardhi mara wastani wa asilimia ya riba inayotolewa na Benki za Kibiashara kwa akiba ya muda maalum ya miezi kumi na miwili (12) wakati wa kupoteza ardhi.

17.   Posho ya usafiri

   Posho ya usafiri itakuwa gharama halisi ya kusafirisha tani kumi na mbili (12) za mizigo kwa reli au barabara (kutegemea njia ya gharama nafuu) hadi umbali usiozidi kilomita ishirini (20) kutoka mahali pa kuondoshwa.

18.   Ardhi isiyokaliwa

   Posho za usafiri, upangaji na kupoteza faida hazitalipwa kwa ardhi isiyokaliwa wakati maslahi katika ardhi yanapotezwa.

19.   Riba

   (1) Riba za usafiri, upangaji na kupoteza faida Kuu au Mamlaka ya Serikali ya Mtaa pale tu ambapo malipo ya fidia hayakulipwa kwa wakati.

   (2) Kwa ajili ya ukadiriaji wa riba kwenye fidia mayotakiwa "kulipwa kwa wakati" maana yake ni kulipa fidia katika kipindi cha miezi sita baada ya ardhi mayohusika kutwaliwa au hakimiliki kubatilishwa.

   (3) Endapo kiwango cha fidia hakilipwi miezi sita (6) baada ya ardhi kutwaliwa au hatimiliki kubatilishwa riba italipwa kwa wastani wa asilimia ya riba mayolipwa na Benki za kibiashara kwenye akiba za muda maalum hadi fidia itakapolipwa.

20.   Kupewa taarifa ya kudai fidia

   Pale ambapo fungu la 4 na la 6 yanahusika, Kamishna atatoa taarifa, kwa fomu iliyoko katika Jedwali la Kwanza, kwa Halmashauri ya Kijiji na watu wote wanaokalia ardhi kwa hakimiliki ya kimila au hakimiliki isiyo asili kwenye eneo la ardhi linalohusika na taarifa ya kuhawilisha ardhi ya kijiji au, kwa kadiri itakavyokuwa, taarifa ya kutangaza ardhi yenye madhara katika Halmashauri ya Kijiji na watu wote waliotajwa katika kanuni hii walete madai yao ya fidia.

21.   Madai ya fidia

   Madai ya fidia yatawasilishwa kwa fomu iliyopo katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi katika kipindi kisichopungua siku sitini baada ya kupokelewa taarifa iliyotajwa katika kanuni ya 20.

22.   Msaada wa kutayarisha madai ya fidia

   Afisa Mteule, kutokana na ombi la Afisa wa Kijiji ambacho ardhi yake imetolewa taarifa chini ya fungu la 4 la Sheria kuhusu kuhawilisha ardhi ya kijiji, au taarifa chini ya fungu la 6 la Sheria kuhusu kutangaza ardhi ya kijiji kuwa ardhi yenye madhara atalazimika kusaidia kijyi hicho na watu wanaokalia maeneo ambayo yametolewa matangazo namna ya kuandaa na kuwasilisha madai ya fidia.

23.   Kukubali madai ya fidia

   (1) Kamishna, katika kipmdi kisichozidi siku tisini kutoka tarehe madai yalipowasilishwa, ataamua ama ayakubali au ayakatae maombi hayo au sehemu yake.

   (2) Endapo Kamishna atakubali madai yoyote ya fidia yaliyowasilishwa chini ya kanuni ya 21, basi atatoa taarifa kwa Waziri.

   (3) Katika kipindi kisichopungua siku ishirini na moja tangu Waziri kupokea taarifa, Kamishna atafanya utaratibu wa kumwezesha mdai alipwe fidia.

24.   Usuluhishi kuhusu madai ya fidia

   (1) Endapo Kamishna ataamua kutokubali madai ya fidia iwapo mdai na Kamishna wataafikiana, madai hayo yanaweza kurejeshwa kwa mtu atakayeteuliwa na Waziri kuwa msuluhishi wa suala hilo.

   (2) Endapo msuluhishi atafaulu kupatanisha pande husika, atampeleka Waziri taarifa ya upatanisho huo, na Kamishna katika kipindi cha siku ishirini na moja tangu Waziri apokee taarifa kutoka kwa msuluhishi, atafanya utaratibu wa kumwezesha mdai alipwe fidia.

   (3) Endapo msuluhishi, baada ya siku zisizopungua tisini za majadiliano kati ya pande husika, atashindwa kuzisaidia kufikia makubaliano katika suala la madai ya fidia au endapo pande zote husika au upande mmoja wapo hautaki kupeleka suala la madai kwa msuluhishi, basi suala hilo litapelekwa kwenye Mahakama yenye mamlaka.

25.   Aina za Fidia

   (1) Fidia kwa mujibu wa fungu la 4 na la 6 la Sheria na Kanuni ya 13 yaweza kutolewa kwa namna au mojawapo ya namna zifuatazo:–

   (a)   ardhi inayofanana kwa ubora, ukubwa na uwezo wa kuzalisha kama ardhi iliyopotea;

   (b)   jengo linalofanana kwa ubora, ukubwa na matumizi kama jengo lililopotea;

   (c)   mimea na miche;

   (d)   fursa ya kutumia mali za jumuiya;

   (e)   kiasi cha fedha sawa na thamani ya uboreshaji usiohamishika wa ardhi iliyohawilishwa au ardhi iliyotangazwa kuwa ardhi yenye madhara, au malipo ya fidia kwa kupunguza eneo la ardhi ama kwa upotevu au uharibifu wa ardhi ambayo inaweza kutumika kuzalisha, au malipo kwa ajili ya usumbufu uliosababishwa na uhawilishaji wa ardhi au ardhi kutangazwa kuwa ardhi yenye madhara;

   (f)   kupewa mara kwa mara nafaka na vyakula vingine mbalimbali kwa kipindi kitakachowekwa;

   (g)   namna nyingine za fidia zinazoweza kukubalika kati ya mdai na Kamishna.

SEHEMU YA IV
USIMAMIZI WA PAMOJA WA ARDHI YA KIJIJI

26.   Pendekezo la Usimamizi wa pamoja wa Ardhi ya Kijiji

   Pendekezo la usimamizi wa pamoja wa ardhi ya kijiji baina ya vijiji viwili, au kijiji na Halmashauri ya Wilaya au mamlaka ya mji, laweza kutolewa na Kamishna wa Ardhi kwa Halmashauri za Vijiji na Halmashauri za Wilaya au Halmashauri ya Mji, au laweza kutolewa na halmashauri ya kijiji kwa halmashauri ya kijiji kingine au mamlaka yoyote ya mtaa, au laweza kutolewa kwa halmashauri ya kijiji ambacho inapendekezwa kuundwa kwa usimamizi huo wa pamoja nayo.

27.   Kupigia kura pendekezo la Usimamizi wa Pamoja wa Ardhi ya Kijiji

   Pendekezo lililotajwa katika Kanuni ya 2 lazima lifikiriwe na lipigiwe kura na halmashauri za vijiji na halmashauri za mamlaka za mitaa zinazohusika.

28.   Kukataliwa kwa pendekezo la Usimamizi wa Pamoja wa Ardhi ya Kijiji

   Endapo pendekezo litakataliwa na halmashauri ya kijiji au mamlaka ya mtaa, lazima kipindi kisichopungua miezi mitatu kipite ndipo pendekezo hilo au pendekezo lenye marekebisho laweza kuletwa lifikiriwe tena na halmashauri ya kijiji au halmashauri ya mamlaka ya mtaa iliyokataa pendekezo la awali.

29.   Uteuzi wa Kamati ya pamoja

   Halmashauri za vijiji na mamlaka za mitaa zinazopiga kura kukubali uundaji wa mpango wa usimamizi wa pamoja, kila moja itateua watu wasiopungua watatu na wasiozidi watano kuwa wajumbe wa Kamati ya Pamoja ili waandae Mpango wa Usimamizi wa Pamoja.

30.   Tafakari ya Rasimu ya Mpango wa Usimamizi pamoja

   Baada ya Kamati ya Pamoja kuafikiana kuhusu rasimu ya Mpango wa Usimamizi wa Pamoja, itapeleka rasimu hiyo katika mkutano wa kijiji na halmashauri ya mamlaka ya mtaa husika kwa ajili ya vyombo hivyo kuufikiria na kuupigia kura mpango huo.

31.   Marekebisho ya Rasimu ya Mpango wa Usimamizi wa Pamoja

   Mkutano wa kijiji na halmashauri ya mamlaka ya mtaa vinaweza kupendekeza marekebisho katika rasimu ya Mpango wa Usimamizi wa Pamoja, na mapendekezo yoyote ya marekebisho yatawasilishwa kwa Kamati ya pamoja ili yafikiriwe.

32.   Makubaliano ya Mpango wa Usimamizi wa Pamoja

   Mpango wa Usimamizi wa pamoja hautatekeleza hadi hapo kila kijiji na kila mamlaka ya mtaa husika katika mpango huo waafiki vipengele vya mpango huo na wawe wamepiga kura ya kuupokea mpango huo.

33.   Kamati ya Pamoja inawajibuka kwa uendeshaji wa usimamizi wa Pamoja

   Kamati ya Pamoja iliyoundwa kuandaa Mpango wa Usimamizi wa Pamoja itakuwa na jukumu la utekelezaji wa Makubaliano ya Matumizi ya Pamoja ya Ardhi na itakutana si chini ya mara moja kila miezi mitatu kuhakikisha kunakuwepo uendeshaji madhubuti na rahisi.

34.   Vipengele vinavyoelekeza uendeshaji wa Kamati ya pamoja

   Kamati ya Pamoja iliyoundwa chini ya Kanuni hizi itaongozwa na kufuata miongozi inayoongoza shughuli za kamati zilizowekwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya).

35.   Yaliyomo katika mpango wa usimamizi wa Pamoja

   Mpango wa Usimamizi wa Pamoja utashughulikia usimamizi wa ardhi ya kijiji kinachohusika na bila ya kuathiri ujumla wa kanuni hii, mpango huo waweza kuwa na vipengele vinavyohusu:

   (a)   mipango na uratibu wa ujenzi na matumizi ya majengo kwenye ardhi;

   (b)   uzoaji wa takataka katika ardhi;

   (c)   ulinzi na hifadhi ya maeneo yoyote ya hifadhi ya misitu kwenye ardhi ya kijiji, au kwenye maeneo mengine yenye misitu inayosimamiwa na kijiji, au kwenye maeneo mengine maalum ya ardhi ya kijiji;

   (d)   utoaji wa misaada kitaaluma ili kukisaidia katika usimamizi wa ardhi ya kijiji;

   (e)   kuchangia gharama za usimamizi wa ardhi ya kijiji pale ambapo gharama za usimamizi zimeongezeka kutokana na shughuli za maendeleo yanayotokea katika halmashauri ya wilaya au ya mamlaka ya mji;

   (f)   muda usiozidi miaka mitatu, ambapo mpango wa usimamizi wa pamoja utadumu;

   (g)   taratibu za kusuluhisha tofauti baina ya pande shiriki za Mpango wa usimamizi wa Pamoja.

SEHEMU YA V
DAFTARI LA ARDHI KIJIJI

36.   Sehemu ya Daftari

   Daftari litagawanywa katika sehemu zifuatazo–

   (a)   Sehemu A Cheti cha Ardhi ya Kijiji;

   (b)   Sehemu B Daftari la Hati;

   (c)   Sehemu C Daftari Bayana la Kutahadharisha.

37.   Cheti cha Ardhi ya Kijiji

   (1) Cheti cha Ardhi ya Kijiji kitakuwa katika fomu iliyowekwa katika Jedwali la Kwanza na itahifadhiwa katika sehemu tofauti ya Daftari.

   (2) Kumbukumbu pekee zinazoweza kuingizwa kwenye Cheti cha Ardhi ya kijiji ni:

   (a)   marekebisho, anayoagiza Kamishna yafanywe, ili kuweka kumbukumbu za mabadiliko ya mipaka ya ardhi ya kijiji;

   (b)   kumbukumbu zinazoonyesha vipande vya ardhi viliyomegwa au vilivyoongezwa kwenye ardhi ya kijiji chini ya fungu la 4 na la 5 la Sheria;

   (c)   kumbukumbu zinazoonyesha maeneo ya ardhi ya kijiji yaliyotangazwa kuwa ardhi yenye madhara chini ya fungu la 6 la Sheria.

38.   Daftari la Hati

   (1) Daftari la Hati litakuwa ni Daftari lenye:

   (a)   kumbukumbu ya hatimiliki za kimila sehemu ya 1 ya Daftari la Hati;

   (b)   kumbukumbu ya hakimiliki zisizo asili sehemu ya 2 ya Daftari la Hati;

   (c)   kumbukumbu zote za uhamishaji na shughuli zinazohusiana na hakimiliki za kimila na hakimili zisizo za asili, ikiwa ni pamoja na ilani zozote zilizoingizwa kwenye daftari la Hati-Sehemu ya 3 ya daftari la Hati.

   (2) Afisa atasajili kwenye sehemu husika ya Daftari la Hati kwa namna ilivyoelekezwa na Kanuni hizi nyaraka zote zilizowasilishwa kwake katika fomu zilizoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza.

39.   Daftari Bayana la kutahadha risha

   (1) Daftari Bayana la kutahadharisha litakuwa daftari lenye:

   (a)   nyaraka za kurejesha hakimiliki ya kimila;

   (b)   amri za kutekeleza ardhi;

   (c)   amri za kuhakilisha kwa muda hakimiliki ya kimila;

   (d)   taarifa zinazohusu kulipa au kutolipa kodi ya pango, kodi, faini na malipo mengine yapaswayo kulipwa kwa taasisi yoyote ya umma kwa kuhusiana na hakimiliki ya kimila au hakimiliki isiyo asili au ya kukalia ardhi ya kijiji;

   (e)   nyaraka zinazoweka kumbukumbu za maelezo ya mpango wa usimamizi wa pamoja;

   (f)   kumbukumbu inayoweka uamuzi wa Mkutano wa Kijiji au Halmashauri ya Kijiji au chombo kingine chochote chenye mamlaka ya kuamua kwamba eneo la ardhi ya kijiji litahifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya misitu, usimamizi wa wanyama pori au vinginevyo yametengwa kwa malengo ya hifadhi;

   (g)   kumbukumbu inayoweka uamuzi wa mkutano wa Kijiji kwamba sehemu ya ardhi ya kijiji imetengwa kama ardhi ya pamoja ya kijiji kwa mujibu wa fungu la 13 la Sheria.

   (2) Afisa atasajili kwenye Daftari Bayana la kutahadharisha kwa namna ilivyoelekezwa na Kanuni Hizi, nyaraka zote zinazohusiana na masuala yaliyorejewa kwenye kanuni hii, zitakazowasilishwa kwake kwenye fomu zilizoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza.

40.   Watu wanaostahili kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya usajili

   Waraka kwa ajili ya usajili sharti uwasilishwe na mtu anayedai maslahi kutokana na waraka huo, au mwakilishi wake, na Afisa anaweza kuhoji ili ajiridhishe na utambulisho na maslahi ya mtu anayewasilisha waraka au kama ni mwakilishi mamlaka yake.

41.   Taarifa za Usajili

   (1) Usajili utahusisha hatua ya Afisa kuweka kwenye jalada waraka uliotolewa kwa mujibu wa kanuni ya 13, na kumkabidhi mtu anayeleta waraka kwa ajili ya usajili nakala ya waraka huo (ambayo mtu yule anatakiwa kuleta) baada ya nakala hiyo kuthibitishwa na Afisa kwamba ni nakala halisi ya waraka huo.

   (2) Saini ya Afisa kama ilivyoelezwa katika ibara (1) ya kanuni hii, kwenye nyaraka iliyosajiliwa na nakala yake, itakuwa ushahidi tosha wa usajili.

42.   Utoaji wa namba na hifadhi ya nyaraka zilizosajiliwa

   Afisa atatoa namba zinazofuatana kwa kila waraka unaohifadhiwa na kuwekwa kumbukumbu kwenye waraka inayoonyesha tarehe ya usajili na jina la mtu aliyewasilisha waraka huo na Afisa atahifadhi nyaraka katika sehemu husika za Daftari la Hati kwa mpangilio kadri anavyozipokea.

43.   Kumbukumbu kimaandishi iliyoambatanishwa na waraka uliosajiliwa

   Kumbukumbu iliyosainiwa na Afisa itaambatishwa kwenye kila waraka iliyosajiliwa ikinukuu maelezo mafupi ya usajili, kumbukumbu hiyo itakuwa ushahidi tosha wa awali kwamba waraka umesajiliwa kama ipasavyo.

44.   Kitabu cha muhtasari

   Afisa atatunza kitabu kitakachoweka muhtasari wa kumbukumbu zilizomo kwenye Daftari la Hati, na kwa kila cheti kitakachosajiliwa, ataingiza katika kitabu hicho namba ya usajili, jina la mwenye au wenye cheti, tarehe ya cheti na tarehe usajili na ukurasa tofauti wa kitabu hicho utatumika kuweka kumbukumbu zinazohusu cheti kilichosajiliwa.

45.   Mwenye haki kutaarifiwa

   (1) Mwenye hakimiliki ya kimila au hakimiliki isiyo asili anayefanya uhamishaji au shughuli kwenye ardhi au mtu mwingine yeyote anayehusika kwenye shughuli hiyo, aweza katika kipindi cha miezi miwili cha kukamilisha shughuli hiyo, kuwasilisha kwa afisa nyaraka za ushahidi wa shughuli hiyo.

   (2) Endapo shughuli yoyote ya ardhi matakiwa kupata kibali cha mwanandoa, ushahidi wa kimaandishi wa shughuli hiyo lazima uambatishwe na ushahidi wa kimaandishi wa kibali hicho au vibali hivyo vimetolewa.

46.   Jukumu la Afisa kwenye shughuli za ardhi

   Endapo ushahidi kimaandishi wa shughuli za ardhi unapelekwa kwa Afisa chini ya Kanuni ya 45 na mtu anayehusika na shughuli hiyo ya ardhi ambaye si mwenye hakimiliki ya kimila au hakimiliki isiyo ya asili, basi Afisa

   atampelekea taarifa yule mwenye hakimiliki kuhusu jambo hilo na hatachukua hatua zozote za kusajili shughuli hiyo ya ardhi mpaka mwenye hakimiliki au mwakilishi wake atoe ushahidi wa kutosha kwamba alijiingiza katika shughuli hiyo ya kibiashara kwa hiari yake na kwamba alijua kwa ufasaha matokea ya shughuli hiyo.

47.   Shughuli za miliki za ardhi

   (1) Afisa atawajibika–

   (a)   kujiridhisha kwamba nyaraka zote muhimu zinazohusiana na shughuli yoyote ya ardhi, zimewasilishwa;

   (b)   kuambatisha nakala ya ushahidi kimaandishi kuhusu shughuli ya ardhi inayohusika (itakayotolewa na mwenye hakimiliki ya kimila au mwenye hakimiliki isiyo asili) kwenye waraka unaohusiana nayo, na kuipa namba ya nakala hiyo;

   (c)   kuambatanisha kumbukumbu kimaandishi iliyosainiwa na Afisa kwenye waraka iliyorejewa katika ibara ya (b) hapo juu, ikinukuu kwa muhtasari yaliyomo kwenye shughuli ya ardhi, na kumbukumbu ambayo itakuwa ushahidi tosha wa awali kwa shughuli ya ardhi imesajiliwa ipasavyo;

   (d)   Kuandika kwenye ukurasa wa Kitabu cha Muhtasari ambapo kwa mujibu wa kanuni ya 37, kumbukumbu za waraka unaohusiana na shughuli ya ardhi husika zimewekwa zikionyesha namba ya usajili wa shughuli ya ardhi, tarehe ya shughuli ya ardhi na tarehe ya usajili shughuli ya ardhi.

   (2) Afisa hatakuwa na uwezo wa kuambatisha ushahidi wowote kimaandishi kwa shughuli ya ardhi kwenye waraka uliyosajili, au kuingiza kwenye Kitabu cha Muhtasari, taarifa yoyote inayohusu shughuli ya ardhi, endapo ushahidi huo kimaandishi haukuambatishwa na vibali vilivyorejewa katika kanuni ndogo ya (2) ya kanuni ya 45 popote pale ambapo vibali hivyo vinatakiwa, na hatua yoyote ya Afisa kinyume cha hali itakuwa batili.

48.   Kipaumbele

   (1) Shughuli katika ardhi inayomilikiwa kwa waraka uliyosajiliwa zitakuwa na kipaumbele baina yao kwa mpangilio wa tarehe na saa zilipopata usajili kwa mujibu wa kanuni ya 42.

   (2) Shughuli ya ardhi iliyosajiliwa kwa mujibu wa kanuni ya 42, itapewa kipaumbele juu ya shughuli nyingine ambayo haikusajiliwa, hata kama shughuli iliyosajiliwa ilikamilishwa, kabla au baada ya shughuli isiyosajiliwa.

49.   Afisa aweza kukataa kusajili nyaraka

   Afisa aweza kukataa kusajili au kuingiza katika Daftari waraka wowote kama:

   (a)   haikuandaliwa katika fomu iliyoainishwa au;

   (b)   fomu au waraka mwingine umeharibika kwa kuchanwa, kuchafuka, kufifia maandishi au kuharibika kiasi cha kutoweza kueleweka tena; au

   (c)   waraka huo unaonyesha kuongezwa maneno kati ya mistari ya waraka, au nafasi kuwa tupu, maneno kufutwa au kubadilishwa isipokuwa tu kama waliowasilisha nyaraka hizo wamesaini au wameweka majina yao kwa mkato mahali penye maneno yaliyoongezwa palipo patupu palipofutwa au kubadilishwa na katika hali hiyo Afisa ataingiza katika rejesta kumbukumbu ya maneno kuongezwa, mahah kuacha patupu, kufutwa au kubadilishwa.

50.   Uwezo wa Afisa kusahihisha makosa

   Endapo mtu yeyote atadai kuwepo kosa au upungufu ulifanyika kwenye usajili au upungufu kwenye daftari umesababishwa na udanganyifu au kosa Afisa akiridhika kuwa dai limethibitisha kikamilifu atasahihisha kosa hilo la upungufu au usajili.

51.   Usajili hautaondoa kasoro au kuhalalisha

   Usajili hautaondoa hitilafu yoyote katika waraka uliyosajiliwi au kuhalalisha waraka ambao vinginevyo usingekuwa halali isipokuwa tu kwa kiwango kinachokubalika kwa mujibu wa Sheria na Kanuni hizi.

52.   Daftari laweza kukaguliwa na nakala kupatikana

   Daftari laweza kukaguliwa na kuchunguzwa na mwombaji yeyote wakati wa saa za kawaida za kazi na nakala halisi zilizothibitishwa na Afisa kuwa nakala halisi za wowote uliosajiliwa au sehemu yake vinaweza kupatikana kama vikitakiwa, lakini waraka uliohifadhiwa kwenye daftari au ulioambatishwa kwenye waraka ulisajiliwa na kuhifadhiwa katika daftari hautaruhusiwa kuondolewa katika daftari.

53.   Nyaraka mbadala ya iliyosajiliwa

   Endapo waraka asili uliyosajiliwa umepotea, umechanika au umeteketea, Afisa aweza kuandaa nakala itakayokuwa na maelezo yote kutokana na taarifa katika kumbukumbu zote katika ofisini na vyanzo vingine.

54.   Nakala ya wataka uliyosajiliwa

   (1) Endapo nakala iliyosajiliwa imepotea, imechanika au imeteketea, Afisa aweza, kutokana na maombi ya mmilikaji au mkazi, yakiambatishwa na tamko rasmi kwenye fomu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi, kuandaa nakala yenye maelezo yote yaliyomo kwenye hati asili au hati mbadala iliyosajiliwa.

   (2) Afisa atathibitisha kwenye nakala kwamba ni nakala ya waraka uliosajiliwa.

   (3) Afisa atatangaza ombi hilo kwa gharama ya mwombaji na tangazo hilo litalolewa katika gazeti linalosomeka kwa wingi katika eneo hilo na nakala inayoombwa itatolewa kwa siku thelathini baada ya tangazo.

55.   Kupatikana waraka uliyosajiliwa

   (1) Endapo waraka asili uliyosajiliwa na kupotea ukipatikana, Afisa ataufanyia marekebisho na atafuta hati mbadala iliyosajiliwa.

   (2) Waraka mbadala uliosajiliwa na kututwa utatunzwa katika masjala.

56.   Kupatina nakala ya waraka uliosajiliwa

   (1) Endapo nakala ya waraka uliosajiliwa na kupotea inapatikana, Afisa ataufanyia marekebisho kwa kuingiza taarifa mpya na kufuta nakala mbadala.

   (2) Nakala mbadala iliyofutwa itatunzwa katika masjala.

57.   Nakala ya waraka potevu uliosajiliwa

   Endapo waraka wowote uliosajiliwa chini ya Kanuni hizi, nakala yake iliyothibitishwa na Afisa itakubalika katika ushahidi wa mambo yaliyomo mbele ya Mahakama zote Tanzania kwa kuzingatia tofati za haki na kisheria.

58.   Nakala iliyothibitishwa ya waraka uliosajiliwa kukubalika katika kesi ya madai

   Kila nakala iliyothibitishwa ya waraka wowote uliosajiliwa na inayoonekana kwamba imesainiwa na Afisa itapokeleka kama ushahidi katika kesi yoyote ya madai mbele ya Baraza au Mahakama bila uthibitisho wa usahihi wa nakala hiyo au usahihi wa saini hiyo, isipokuwa tu kama itadaiwa kwamba waraka asili umeghushiwa au kwamba nakala inayoonekana kusainiwa na Afisa in ya kughushi na siyo sahihi.

59.   Matumizi ya nakala iliyothibitishwa ya waraka uliosajiliwa katika kesi za madai

   Katika kesi ya madai, upande unaopendekeza matumizi ya nakala iliyothibitishwa ya waraka uliosajiliwa utatoa nakala ya waraka huo kwa upande mwingine na nakala hiyo itapokelewa katika ushahidi endapo Baraza au Mahakama itaridhika kwamba nakala imetolewa mapema kabla upande unaopinga kukagua daftari asili ilikopatikana nakala.

60.   Muda wa Masjala kuwa wazi

   Masjala itakuwa wazi kwa umma kwa siku, saa na muda kadri Halmashauri ya Kijiji itakavyoamua.

SEHEMU YA VI
USULUHISHI WA MASLAHI NA MIPAKA KATIKA ARDHI

61.   Taarifa kwa pande zinazohusika

   Kwa malengo ya fungu la 54 la Sheria, Kamati kwa mujibu wa fungu la 7(2) Sheria itatoa taarifa kwa kutumia fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi.

62.   Kuweka mipaka

   (1) Kamati itatembelea ardhi inayohusika na uamuzi wa maslahi na mipaka katika ardhi ikitafuta, ikibaini/ikithibitisha, ikiamua na kuweka mipaka ya ardhi.

   (2) Katika kuweka mipaka, Kamati itatumia alama za mipaka ambazo kwa kawaida zinatumika kwenye maeneo husika, ikiwa ni pamoja na mipaka ya njia, mifereji, uzio katani na mimea mingine na mawe.

   (3) Katika kuweka alama za mipaka, sehemu ya mzunguko, kona na mabadiliko mengine ya mwelekeo yatapewa umuhimu, na kati ya sehemu hizo alama zitawekwa kwa umbali ambao utaziwezesha kuonekana kwa urahisi alama moja baada ya nyingine.

63.   Uthibitisho wa mipaka

   Kamati, mwombaji, na angalau watu wazima wawili ambao ni wakazi wa eneo waliohudhuria ukaguzi wa ardhi, watathibitisha usahihi wa mipaka kwa kusaini katika fomu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi.

64.   Kusafisha na kuweka alama kwenye mipaka

   Gharama zinazohusiana na shughuli zilizotajwa katika Kanuni ya 61 ya Kanuni hizi zitalipwa na mwombaji au kama itakavyokubalika kati ya Halmashauri ya Kijiji na mwombaji.

65.   Kutunza mipaka

   Utunzaji wa mipaka utakuwa jukumu la wenye hakimiliki ya kimila.

66.   Kipimo cha Upimaji

   Kipimo cha upimaji kitakuwa mita.

67.   Matavarisho ya Muhoro

   (1) Katika utaratibu wa kuweka mipaka ya ardhi Kamati itaandaa mchoro wa ardhi inayohusika.

   (2) Mchoro utapaswa–

   (a)   utachorwa na kuambatishwa na fomu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la kanuni hizi;

   (b)   utachorwa kwenye karatasi inayodumu muda mrefu kwa kutumia kifaa cha kuandikia kitakachoweka alama ya kudumu;

   (c)   utakuwa wa mistari inayounganishwa na kufanya umbo lililofungwa;

   (d)   kuonyesha sambamba na mstari, umbali uliopimwa katika mita, kati ya alama moja na nyingine zilizochorwa kwa alama za msalaba;

   (e)   kuonyesha majina ya wakazi wa vipande vyote vya ardhi jirani;

   (f)   kuonyesha mwelekeo unaokaribia kaskazini;

   (g)   kuonyesha alama za rejea zinazoonekana na za kudumu kama zipo, kwenye ardhi au karibu, ikiwa ni pamoja na njia za miguu, barabara, mapito ya mifugo, mito, majengo ya kudumu, majabali na miti.

68.   Taratibu za upimaji

   (1) Mipaka itapimwa kwa kutumia futi kamba na haitakuwa lazima kuchora mchoro kwa vipimo au kubainisha ukubwa wa eneo.

   (2) kama mwombaji anataka kujua ukubwa wa ardhi husika aweza kufanya taratibu na kulipa gharama za huduma ya Mpima Ardhi.

69.   Kuweka kumbu-kumbu ya haki za njia

   Haki ya njia itaonyeshwa katika mchoro kwa mistari ya nukta na itafafanuliwa wazi wazi.

70.   Mgao wa mchoro

   Kamati, itatayarisha nakala tatu za mchoro ambazo zitagawiwa kwa Kamati, mwombaji na Halmashari ya Kijiji.

71.   Kumbu-kumbu za uamuzi wa ntaslahi na mipaka katika ardhi

   (1) Kumbukumbu ya uamuzi wa maslahi na mipaka katika ardhi itatayarishwa kwa kila kipande cha ardhi ambacho kinahusika na dai moja au zaidi na itaonyesha:

   (a)   jina la mdai, au kama kuna zaidi ya mtu mmoja anayedai ardhi hiyo, majina ya wadai wote;

   (b)   aina na kiasi cha maslahi kinachodaiwa katika ardhi;

   (c)   kiasi cha ardhi kinachodaiwa;

   (d)   muda ambao au muda wanaodai maslahi katika ardhi hiyo;

   (e)   mahali na mipaka ya kipande husika cha ardhi;

   (f)   njia na mipaka ya Haki za njia zozote au Haki za fursa ya njia au huduma nyingine za umma zinazodaiwa kuwepo kwenye, juu au chini ya ardhi;

   (g)   Uamuzi wa Kamati ya Uamuzi ya Kijiji au kadri itakavyokuwa uamuzi wa Afisa Mshauri wa Uamuzi wa Kijiji kuhusu dai au madai hapo pamoja na maelezo kwa ufupi ya sababu za uamuzi huo.

   (2) Kumbukumbu ya uamuzi wa maslahi katika ardhi na mipaka lazima iambatishwe na mchoro ulioandaliwa kwa mujibu wa kanuni ya 67.

   (3) Kumbukumbu ya uamuzi wa maslahi ya ardhi na mipaka itakuwa kwenye fomu iliyoonyeshwa kwenye Jedwali la Kwanza la Kanuni Hizi.

72.   Taarifa ya upimaji wa ardhi nayomilikiwa kwa hakimiliki ya kimila inayosajiliwa

   (1) Endapo haki ya kumiliki ya kimila imetolewa baada ya uamuzi wa maslahi na mipaka ya ardhi, na baadaye ardhi ikapimwa, mkazi atatoa taarifa kwa Afisa wa eneo lililopimwa na kuwasilisha ramani iliyothibitishwa.

   (2) Taarifa iliyotolea kwa mujibu wa kanuni ndogo ya kwanza itaandikwa kwenye fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni Hizi.

73.   Namba ya Uthitibisho wa Kipande cha Ardhi

   Kipande cha ardhi ambacho, baada ya uamuzi wa maslahi na mipaka ya ardhi, hakimiliki ya kimila imetolewa na kusajiliwa katika Daftari la Ardhi ya Kijiji, kitaonyesha namba ya pekee ya Utambulisho wa Kipande cha Ardhi (UKA) itakayotolewa na Afisa.

74.   Mgawanyo

   Endapo kunafanyika mgawanyo wa hakimiliki ya kimila iliyosajiliwa, namba ya utambulisho ya awali (UKA) itafutwa na namba nipya ya utambulisho (UKA) itatolewa kwa kila eneo jipya litokanalo na mgawanyo, kwa kutumia fomu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi.

SEHEMU YA VII
MENGINI YO

75.   Waziri aweza kuweka vya juu vya kumiliki ardhi

   (1) Waziri aweza, kwa kuwasiliana na Waziri mwenye dhamana ya kilimo, kwa Amri iliyotangazwa kwenye Gazeti, kuweka kiwango cha juu cha ardhi ambacho mtu yeyote anaweza kukalia kwa hakimiliki ya kimila au hakimiliki isiyo ya asili.

   (2) Katika kutekelelza jukumu lake chini ya kanuni ndogo ya (1), Waziri atazingatia:–

   (a)   taarifa na miongozo yote inayopatikana kuhusu tathmini ya ardhi kuhusu matumizi maalum kwa mkulima mdogo, shughuli za ukulima, za ufugaji na za misitu katika sehemu na maeneno mbalimbali ya uchumi na kilimo Tanzania ili kusukuma maendeleo halisi ya ukulima na matumizi kamili ya ardhi;

   (b)   haja ya kuhimiza na kuhakikisha utunzaji wa mazingira;

   (c)   kuhusiana na ardhi itayotumika kwa maendeleo ya miji, miongozo iliyopo ya ukubwa wa viwanja kwa aina mbalimbali za uendelezaji wa miji kama ilivyoandaliwa na Idara va Mipango Miji;

   (d)   haja ya kusaza ardhi katika kila kijiji kwa ajili ya ugavi wa siku za usoni;

   (e)   mila na desturi zilizopo vijiini katika wilaya au mkoa ambako anapendekeza kuweka viwango vya juu vya ardhi kama mipaka ambayo mwanakijiji yeyote au famili itaruhusiwa kumiliki.

   (3) Viwango vya juu tofauri vya ardhi vyaweza kuwekwa:

   (a)   kwa kila mkoa; na

   (b)   kila wilaya mkoani; na

   (c)   kila kijiji wilayani

   (4) Viwango vya juu vinavyowekwa chini ya kanuni hii vitarejewa mara kwa mara na kurekebishwa inapobidi.

76.   Taratibu za idhini ya viwango vya juu vya kumiliki ardhi

   (1) Mpaka hapo matangazo yatakapotolewa na kutangazwa kwa mujibu wa kanuni ya 74, Halmashauri yoyote ya kijiji haitatoa au kukubali kutoa an kuidhinisha uhamishaji wa hakimiliki ya kimila au kutoa au kuidhinisha utoaji wa hakimiliki isiyo asili katika ardhi ya kijiji au hakimiliki ya kimila zaidi ya hekta ishirini au kiwango itakachomfanya mwanakijiji apate zaidi ya hekta ishirini au kiwango cha juu alichonacho mwanakijiji, bila idhini ya Halmashauri ya Wilaya au kamishna kwa mujibu wa Kanuni hii.

   (2) Maombi yakipokelewa kwa Halmashauri ya kijiji ya kutoa ardhi au kwa hakimiliki ya kimila au kwa hakimiliki isiyo ya asili au ya kuidhinisha utoaji wa hakimiliki isiyo ya asili kwa kiwango cha hekta ishirini na moja (21) hadi hekta hamsini (50), Halmashauri ya kijiji itawasilisha maombi hayo kwenye Halmashauri ya Wilaya yenye mamlaka katika wilaya ambako kijiji kipo, pamoja na mapendekezo yake juu ya maombi hayo na haitaidhinisha maombi hayo isipokuwa kwa maandishi kwamba ameafiki maombi hayo.

   (3) Maombi yakipelekwa kwa Halmashauri ya kijiji ya kutoa ardhi ama kwa hakimiliki ya kimila au kwa hakimiliki isiyo ya asili au ya kuidhinisha utoaji wa hakimiliki isiyo ya asili kwa kiwango kinachozidi hekta hamsini (50), Halmashauri ya kijiji itawasilisha maombi hayo kwa Kamishna pamoja na maendelezo yake juu ya maombi hayo na haitaidhinisha maombi hayo isipokuwa kwa maandishi kwamba imeafiki maombi hayo.

77.   Misingi ya jumla ya usuluhishi

   (1) Katika utekelezaji wa shughui za usuluhishi chini ya Sheria au Kanuni hizi, mtu aliyeteuliwa kutimiza majukumu chini ya fungu la 7 au kanuni ya 16, au Kamati katika kutekeleza majukumu yake chini ya fungu la 54, na halmashauri katika kutekeleza majukumu yake chini ya fungu la 14 na la 60 la Sheria–

   (a)   ataongozwa na misingi ya kutokuwa na upendeleo, usawa na haki, kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, haki na wajibu wa pande zote, mila na sheria za Bunge na utamaduni nchi, na kwa kutia; maanani inavyopaswa vipengele vya Katiba ya nchi, na mazingira ya shauri pamoja na mahusiano na migogoro ya awali baina ya pande husika;

   (b)   wataendesha shughuli za usuluhishi kwa namna watakavyoona inafaa, kwa kuzingatia matakwa ya pande husika, mazingira ya mgogoro na umuhimu wa kufikia usuluhishi wa haraka wa mgogoro;

   (c)   watakuwa na kuwasiliana na pande husika mbalimbali au kwa pamoja;

   (d)   wakati wowote wa uendeshaji wa shauri watatoa mapendekezo kwa mdomo au kwa maandishi, kwa kutoa au bila kutoa sababu,

   (e)   kutokana na usuluhishi, inapodhihirika kwamba kuna vipengele vya mapatano au usuluhishi ambavyo vyaweza kukubalika na pande zote wataandaa dondoo za mapatano au usuluhishi na watawaeleza pande zote dondoo hizo, na baada ya kupokea maoni yao, watarekebisha dondoo kwa kuzingatia maoni hayo.

   (2) Endapo mapatano au usuluhishi umefikiwa na pande zote, kamati au Halmashauri, kadri itakavyokuwa, watatayarisha mkataba wa maandishi, ambapo baada ya kusainiwa na pande zote, utawawajibisha wote.

   (3) Mkataba wa maandishi utathibitishwa na msuluhishi aliyeteuliwa, na zilizothibitishwa za mkataba zitagawiwa kwa pande zote.

78.   Maandalizi ya nyaraka

   Afisa au Msajili wa Wilaya watasaidia katika kuandaa nyaraka na fomu kwa niaba ya halmashauri ya kijiji, Kamati, Halmashauri au mwombaji au mmiliki wa ardhi atakayetokea kutumia haki zake chini ya sheria, ili kurahisisha usuluhishi na usajili wa ugawaji na shughuli za kibiashara za maslahi katika ardhi.

79.   Fomu zita-kazotumika kuhusiana na Sheria na Kanuni hizi

   Fomu zilizoorodheshwa katika Jedwali la Kwanza ndizo fomu zinazopaswa kutumika kwa utekelezaji wa majukumu chini ya sheria na kanuni zinazorejewa nayo.

80.   Mabadiliko ya fomu

   Fomu zilizoorodhesliwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi zaweza kufanyiwa mabadiliko au marekebisho katika lugha ili kukidhi mahitaji ya kila shauri, na mabadiliko yoyote katika fomu ambayo hayagusi mambo ya msingi hayataathiri uhahali wake.

81.   Ada

   Ada zilizotajwa katika safu ya pili ya Jedwali la pili la Kanuni hizi ndizo zitakazokuwa ada zinazotakiwa kulipwa kwa ajili ya shughuli zozote zilizoorodheshwa katika safu ya kwanza ya Jedwali la Pili.

82.   Faini

   (1) Unapotokea uvunjaji wa masharti, kama ulivyoorodheshwa katika safu ya 2 ya Jedwali la Tatu la Kanuni hizi kwa hakikimali ya kimila, Halmashauri ya Kijiji inaweza kutoza faini kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Kanuni hizi.

   (2) Halmashauri ya Kijiji itakuwa na uhuru wa kumtoza mkazi kiasi cha faini ambacho ni pungufu kuliko kilichoko kwenye jedwali lililotajwa.

83.   Ushuhuda wa Kusaini Nyaraka

   Ushuhuda na uandaaji wa nyaraka utafanyika kama ulivyoainishwa katika Fungu la 63 la Sheria ya Ardhi ya Mwaka na fungu 91 hadi 94 la Sheria ya Usajili wa Ardhi, Sura Na. 334.

JEDWALI LA KWANDA
FOMU

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 1

JAMHURI YA MUUGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

AMRI YA KUITWA KWENYE KAMATI YA UAMUZI YA KIJIJI

(Chini ya fungu la 53)

   Kwa: Bwana/Bibi/Bi 1 ........................................................................................

Mkutano wa Kijiji cha ...........................................................................................

Umeidhinisha ombi kuhusu uamuzi kwa eneo maalum la ardhi lililoko ......................

linalokaribia takriban ......................................................... (ukubwa/eneo 2).

   Unaamuriwa kuhudhuriwa wewe binafsi na kutoa ushahidi wakati wa usikilizaji wa uamuzi wa

eneo maalum la ardhi lililotajwa hapo juu. Shauri hilo litasikilizwa ..............................

(mahali) siku ya .................................. tarehe .................. saa ..............................

   Tafadhali zingatia kwamba kutoa maelezo ya uongo katika ushahidi wako kunaweza kusababisha ufunguliwe mashtaka ya jinai.

   Jina la Saini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uamuzi ya kijiji ...................................

   Tarehe: ...........................................................................................................

   Imepokelewa na ..............................................................................................

   Saini: .............................................................................................................

   Tarehe ...........................................................................................................

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

AMRI YA KUWASILISHA NYARAKA MBELE YA KAMATI YA KIJIJI

(Chini ya fungu la 53)

   Kwa: Bwana/Bibi/Bi 1 .......................................................................................

Mkutano wa Kijiji cha ............................................... umeidhinisha ombi la kufanya

uamuzi kwa eneo maalum lililoko ........................................... linalokaribia takriban

............................................................. (ukubwa/eneo 2).

   Unaamriwa kuwasilisha nyaraka wewe binafsi au kupitia mwakilishi wako wakati wa kusikiliza madai yanayohusu uamuzi kwa eneo maalum la ardhi siku ya ..................

Shauri litasikilizwa ............................................ (mahali) tarehe ...........................

saa ....................................................................................................................

   Tafadhali zingatia kwamba kuacha, bila sababu za msingi kuwasilisha nyaraka zinazotakiwa kunaweza kusababisha mashtaka ya jinai yafunguliwe dhidi yako.

   Jina na Saini ya Mwenyekiti, Kamati ya Uamuzi ya Kijiji ....................................

tarehe ................................................................................................................

   Imepokelewa na .............................................................................................

   Saini .............................................................................................................

   Tarehe ..........................................................................................................

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

WITO WA KUHUDHURIA MBELE YA KAMATI YA UAMUZI YA KIJIJI

(Chini ya fungu la 53)

   Kwa: Bwana/Bibi/Bi 1 .......................................................................................

amewasilisha ombi kwa Halmashauri ya Kijiji cha ........................................... kwa

ajili ya uamuzi wa eneo maalum la ardhi ambayo ameiombea hakimiliki ya kimila, lililoko

...................................... linalokaribia takriban .................................. (ukubwa/eneo 2).

   Mkutano wa Kijiji cha .......................................................... umeamua kuanza utaratibu wa uamuzi kwa eneo maalumu la ardhi. Unatakiwa uhudhurie mbele ya kamati hiyo wewe

   binafsi tarehe ................................. saa ........................................ kueleza madai yako.

   Zingatia kwamba endapo hutafika bila sababu za msingi unaweza kuhesabiwa kwamba umefuta madai yako.

   Jina na Saini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uamuzi ya Kijiji ...............................

   Tarehe .........................................................................................................

   Imepokelewa na ............................................................................................

   Cheo ...........................................................................................................

   Tarehe .........................................................................................................

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

WITO WA KUHUDHURIA KUSIKILIZWA MBELE YA BARAZA LA ARDHI LA KIJIJI

(Chini ya fungu la 61)

   Kwa: Bwana/Bibi/Bi 1 .......................................................................................

Unatakiwa uhudhurie mbele ya Baraza wewe binafsi siku ya ...................................

tarehe .................................. saa .............................. kutoa ushahidi na kulisaidia

Baraza katika suala la mgogoro kati ya .................................................................

na ......................................................................................................................

   Tafadhali zingatia kwamba kutoa maelezo ya uongo katika ushahidi wako kunaweza kusababisha mashtaka ya jinai yafunguliwe dhidi yako.

   Jina ...............................................................................................................

   Saini: ............................................................................................................

   Sifa: Mwitishaji Baraza la Ardhi la Kijiji cha ......................................................

   Tarehe ..........................................................................................................

   Imepokelewa na ............................................................................................

   Sifa: .............................................................................................................

   Tarehe: .........................................................................................................

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

KIAPO CHA SHAHIDI

(Chin ya fungu la 56)

   Mimi ...................................................................... ninaapa kwa dhati kwamba ushahidi

nitakaotoa kuhusu suala lililoko mbele ya ................................................... (Kamati/Afisa), utakuwa kweli na kweli tupu na itakuwa kweli tu Mungu nisaidie.

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 6

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

TAARIFA YA KUSUDIO LA KUTANGAZA ARDHI YENYE MADHARA

(Chini ya fungu la 6)

Kumb. Na. .........................

   Mimi ..................................................................................... NINATOA TAARIFA kwamba ninakusudia kulitangaza eneo la ardhi lifuatalo kuwa ardhi yenye madhara:

   (a)   Mahala eneo lilipo .................................................................................

   (b)   Mipaka na ukubwa wa eneo hilo .............................................................

   (c)   Sababu za kutoa tamko ........................................................................

   Tamko litatolewa baada ya siku sitini (60) kuanzia tarehe ya kutangazwa taarifa hii kwenye Gazeti. Watu na mamlaka zote zitakazopewa taarifa hii zaweza kuwasilisha maelezo kwa Kamishna wa Ardhi kuhusiana na tamko lililopendekezwa maelezo ambayo inabidi yawasilishwe katika muda wa siku thelathini tokea tarehe ya kupewa taarifa hii.

   Imetolewa hapa ........................................................ siku ya .........................

tarehe ............................... mwezi wa .............................. mwaka 20 ..................

.........................................
   Waziri wa Ardhi

   Imepokelewa na .............................................................................................

   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha ..........................................................

   Tarehe ..........................................................................................................

   Wakazi kwenye ardhi yenye madhara inayopendekezwa

   Jina na saini/kidole gumba ..............................................................................

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 7

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

TAARIFA YA KUITANGAZA ARDHI YENYE MADHARA

(Chini ya fungu la 6)

Kumb. Na. ..........................

   Mimi ..............................................................................................................
NATAMKA eneo lifuatalo kuwa ardhi yenye madhara.

   (a)   Mahala eneo lilipo .................................................................................

   (b)   Mipaka na ukubwa wa eneo hilo .............................................................

   (c)   Sababu za kutoa tamko ........................................................................

   Taarifa itakuwa na nguvu za kisheria siku thelathini baada ya kutangazwa katika Gazeti.

   Zingatia: Tamko hili ni amri ya kutwaa ardhi iliyotajwa katika tamko hili Fidia italipwa kwa upotevu wowote utakaosababishwa na amri hii kwa mujibu wa Kanuni za Ardhi ya Vijiji. Unawajibika kuwasiliana na Afisa Mtendaji wa Kijiji kuhusu masuala yote yanayohusiana na tamko hili.

   KWA AMRI YA RAIS

..........................................
   Waziri wa Ardhi

   Imetolewa na: ................................................................................................

   Jina na saini/alama ya kidole gumba cha mkazi ................................................

   Tarehe ...........................................................................................................

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 8

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI, 1999

(SURA YA 114)

TAARIFA KUHAWILISHA ARDHI YA KIJIJI KUWA ARDHI YA KAWAIDA AU ARDHI YA HIFADHI

(Chini ya fungu la 4)

Kumb. Na............................

This section of the article is only available for our subscribers. Please click here to subscribe to a subscription plan to view this part of the article.