CHAPTER 358
JUDICATURE AND APPLICATION OF LAWS ACT

[SUBSIDIARY LEGISLATION]

INDEX TO SUBSIDIARY LEGISLATION

   NOTICES

      The High Court (Remuneration of Commercial Court Assessors) Notice

   ORDERS

      The Local Customary Law (Declaration) Order (1963)

      The Local Customary Law (Declaration) (No. 2) Order

      The Local Customary Law (Declaration) (No. 3) Order

      The Local Customary Law (Declaration) Order (1967)

      The Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order

      The Local Customary Law (Declaration) (No. 5) Order

      The Local Customary Law (Declaration) (No. 7) Order

      The Local Customary Law (Declaration) (No. 8) Order

   RULES

      The Arrest, Seizure and Possession (Bailiffs and Fees) Rules

      The Foreign Tribunals (Service of Process) Rules

      The Foreign Tribunals (Taking of Evidence) Rules

      The Criminal Procedure (Arrests and Orders by Telegram) Rules

      The Criminal Procedure (Suspension of Sentence Pending Appeal) Rules

      The Appearances by Officers of the Government Rules

      The Courts Vacations Rules

      The Court Fees Rules

      The Civil Procedure (Appeals in Proceedings Originating in Primary Courts) Rules

      The Court Brokers and Process Servers (Appointments, Remuneration and Discipline) Rules

   RULES OF COURT

      The High Court Registries Rules

      The Language of Courts Rules

      The Commercial Court (Fees) Rules

NOTICES

THE HIGH COURT (REMUNERATION OF COMMERCIAL COURT ASSESSORS) NOTICE

(Rule 5D)

[12th October, 2001]

G.N. No. 250 of 2001

1.   Citation

   This Notice may be cited as the High Court (Remuneration of Commercial Court Assessors) Notice.

2.   Entitlement

   Every assessor of the High Court (Commercial Division) who attends a session pursuant to Rule 5C of the High Court Registries (Amendment) Rules *, shall be entitled to a sum of forty thousand shillings for each whole day or part of the day he is in attandance at such court.

ORDERS

THE LOCAL CUSTOMARY LAW (DECLARATION) ORDER (1963)

(Section 12)

[1st August, 1963]

G.N. No. 279 of 1963

   1. This Order may be cited as the Local Customary Law (Declaration) Order.

   2. The declaration set out in the First Schedule to this Order is hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained therein in the areas subject to the jurisdiction of the Handeni, Kahama, Kondoa, Lushoto, Musoma, Ngara, Nzega and Pangani District Councils.

   3. Subject to the respective modifications set out in the Second Schedule to this Order in relation to the areas of the several district Councils, the declaration set out in the First Schedule to this Order is hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained therein in the areas subject of the jurisdiction of the Buhaya, Kwimba and Ukerewe District Councils.

FIRST SCHEDULE
DECLARATION OF LOCAL CUSTOMARY LAW

SHERIA ZINAZOHUSU HALI YA WATU

MLANGO WA KWANZA

Mahari

Ulipaji wa Mahari - Sheria za Kawaida

   1. Mahari ni malipo ya ng'ombe au mali ya namna nyingine yalipwayo na bwana arusi kwa baba ya binti au mdhamini wake, sababu anataka kumwoa binti yake.

   2. Kwa kufuata sheria za uvunjaji wa sheria mzazi anaweza kuadhibiwa kwa kutoa ruhusa binti yake kuolewa ili hali hajavunja ungo.

   3. Kabla binti hajafika umri wa miaka 21 hawezi kuolewa bila idhini ya baba yake au mdhamini wa baba yake.

   4. Baada ya kufikia umri wa miaka 21 binti yu huru kuolewa.

   5. Ulipaji wa mahari si jambo la lazima katika kuthibitisha ndoa.

   6. Malipaji ya mahari ni juu ya bwana arusi mwenyewe ingawaje jamaa zake wanaweza kumsaidia katika kutimiza wajibu wake.

   7. Mtu aliye na haki ya kupokea mahari ni baba ya bibi arusi au mrithi wake wa halali bila kujali kama ni mwanamke au mwanamume isipokuwa kama mrithi ni binti ambaye analipiwa mahari.

   8. Iwapo kwa kosa mahari yamelipwa kwa mtu ambaye hana haki kupokea, bwana arusi itambidi kulipa tena na kumpa mtu yule ambaye ana haki hiyo ka kama akitaka kuoa binti. Bwana arusi anaweza kumshtiaki yule mdanganyifu ili amrudishie mali yake.

   9. Lakini ikiwa mpokeaji wa mahari ni mmoja katika wazazi wa kuumeni wa bibi arusi na ikibainika kwamba yuko ndugu mwingine ambaye ndiye ingelibidi apokee mahari hayo, bwana arusi hawezi kuwa na lawama juu ya kosa hilo na shauri litabidi lijadiliwe kati ya ndugu wanaohusika.

Kima cha Mahari

   10. A. Sheria zote zinazoweka mipaka ya kima cha mahari ni lazima zifutwe.

   B. Kiasi cha mahari kinachohitajiwa ni lazima kifikiriwe na kifuatwe na uwezo wa bwana arusi.

   11. A. Katika jimbo la Kati, la Tanga, la Nyanda za Juu, la Tabora, la Shinyanga, la Mara, la Mwanza. la Kigoma na la Kilimanjaro thamani ya sarufu badala ya ng'ombe na mbuzi imekubaliwa kama ifuatavyo:–

   Ng'ombe jike 1 kwa mbuzi 5 au kondoo 5

   Ng'ombe jike 1 kwa Shilingi 100/-

   Fahali 1 kwa Shilingi 90/-

   Mbuzi 1 kwa Shilingi 20/-

   Kondoo 1 kwa Shilingi 20/-

   B. Kwa ajili ya ng'ombe wa Kiankole huko Jimbo la Ziwa Magaribi ni:–

   Ng'ombe jike 1 kwa mbuzi 5 au kondoo 5

   Ng'ombe jike 1 kwa Shilingi 400/-

   Fahali 1 kwa Shilingi 200/-

   Mbuzi 1 kwa Shilingi 40/-

   Kondoo 1 kwa Shilingi 40/-

Kubalidili kwa Ng'ombe waliolipwa kwa Mahari

   12. Baada ya baba ya bibi arusi kwisha chagua na kupokea wanyama ambao ndio mahari na arusi ikiisha fanyika hatakuwa na haki ya kudai kubadilisha mnyama hata kama mnyama huyo ana kasoro ya namna yo yote na bila kujali chanzo cha kifo cha mnyama huyo.

Malipo ya Desturi pasi ya Mahari

   13. Malipo mengine ya kidesturi kuhusikana na arusi ni zawadi ambazo hazirudishwi. Ni vitu vile tu ambavyo lazima virudishwe iwapo mahari yatarudishwa, ndivyo vitakavyohesabiwa kama sehemu ya mahari.

Sheria za Kawaida za Ulipaji wa Mahari

   14. Ni juu ya baba ya bibi ya arusi na bwana arusi mwenyewe kuona kwamba mahari yamelipwa mbele ya mashahidi zaidi ya mmoja kutoka kila upande.

   15. Wanyama, na/au mali yo yote ilipwayo kwa mahari ni mali ya yule mwenye haki ya kupokea ambaye hawezi kulaumiwa kwa kuzitumia au kuziuza.

   16. Mtoto wa wanyama hao anakuwa ni mali ya mwenye haki ya kupokea mahari na hawezi kuhesabiwa kama sehemu ya mahari ambayo yahajalipwa.

   17. Iwapo baba atapokea mahari toka kwa wachumba wawili wa binti yake kwa wakati mmoja, anastahili kutozwa faini isiyopungua shilingi 100/-. Baba ya msichana ni lazima arudishe sehemu yote iliyolipwa na mchumba wa kwanza kabla ya kupokea malipo yo yote toka kwa mtu mwingine.

   18. Iwapo mwanamke amewekwa kinyumba, ndugu ambaye anastahili kupokea mahari kwa niaba yake, haruhusiwi kufanya mashauri yoyote juu ya kuolewa kwa mwanamke huyo na mtu mwingine, na wala huyo ndugu hana ruhusa kupokea malipo ya kwanza ya mahari mpaka yule mwanamke amehama kutoka katika nyumba ya mpenzi wake. Atakayevunja sheria atastahili kulipa faini isiyopungua shilingi 100/-.

   19. Kila moja ya pande mbili zinazohusika na mipango ya arusi, ina haki ya kuvunja mapatano wakati wowote kabla ya arusi kufanyika.

Mahari ilipwayo na Ndugu wa Kuumeni au Kikeni

   20. Jamaa inayotokana na mahari ilipwayo na baba, ndugu wa kuumeni au toka kwa bwana arusi mwenyewe huitwa nyumba ya kuumeni. Jamaa inayotokana na mahari iliyolipwa na dngu wa mama wa bwana arusi huitwa nyumba ya kuukeni.

   21. Iwapo mjomba anataka na baba bnakubali, basi huyomjomba anaweza kumpa mpwa wake mahari yote au sehemu ya kumsaidia mahari hiyo. Vivyo hivyo, mama anaweza kumsaidia mtoto wake katika ulipaji wa mahari kutokana na vitu alivyorithi kwa baba yake.

   22. Watoto kutoka katika hiyo nyumba ya kuukeni hufuata ukoo wa baba yao, lakini kuhusikana na mabinti wakati wanapoolewa ni jambo la kawaida kwa baba ya bibi arusi kutoa sehemu ya mahari na kuwapa nduguze wa kuukeni ambao walimsaidia yeye wakati wa kuoa; lakini hilo si deni linaloweza kufikishwa kwa hakimu.

Mahari ilipwayo baada ya Baba wa Binti kufariki (kama hakuna Hati ya Wosia)

   23. A. Nyumba ya Mke Mmoja

   Iwapo binti anaolewa baada ya baba yake kufariki, mahari yake hupokelewa na mrithi wa haki wa marehemu.

   B. Nyumba ya Wake Waliopalikwa.

    (I)   Iwapo binti anaolewa baada ya baba yake kufariki, mahari yake hupokelewa na kaka yake mkubwa toka nitoke.

   (II)   Iwapo mmoja miongoni mwa wajane hana watoto wa kiume mahari ya binti wake hupokelewa na ndugu yake wa kiume ambaye wamechangia baba na ambaye ndiye mrithi wa jamaa hiyo yote.

   (III)   Iwapo katika jamaa hiyo kuna mabinti watupu, basi mama na mlinzi mwenzake ndio wanaopokea mahari.

   24. Iwapo bibi arusi ni mtu mzima (mwenye miaka 21 au zaidi) na hana ndugu wa kiume wanaoweza kupokea mahari yake, basi mahari yanaweza kupokelewa na rafiti yeyote wa nyumbani kwao lakini hupokea mahari hiyo kama mdhamini tu, na mwenye mali ni yule mwanamke.

   25. Iwapo kuna dada wawili ambao hawana dngu ye yote anayeweza kupokea mahari, basi kila mmoja wao anaweza kupokea mahari ya mwingine.

NAMNA YA KULIPA MAHARI

   A. Mahari ilipwayo yote kabla ya Ndoa

   26.   (I)   Mahari yote inaweza kulipwa mara moja kabla ya ndoa.

      (II)   Mahari yanaweza kulipwa kwa sehemu sehemu na kumalizwa kabla ya ndoa.

   27. Iwapo bwana arusi akishindwa kulipa mahari yote mara moja, kwa kawaida hupewa muda mfupi tu kumaliza kulipa kabla ya ndoa.

   28. Kama mahari ni ng'ombe na kama mnyama mmoja akifa kabla mahari yote hayajamalizwa ni juu ya bwana arusi kutafuta mnyama mwingine, lakini kama mnyama akipotea tu basi hiyo ni hasara ya baba wa binti.

   B. Mahari ilipwayo kwa sehemu sehemu kabla na baada ya Ndoa

   29. Arusi hufanyika baada ya kulipwa kwa sehemu ya kwanza ya mahari. Si desturi kuweka kima na tarehe za ulipaji baada ya arusi.

   30. Kama mume akichelewesha malipo, baba wa binti ana haki ya kudai barazani malipo, baba wa binti ana haki ya kudai barazani malipo ya sehemu zilizobaki. Nis juu ya baraza kufikiri juu ya wakati uliopita tangu malipo ya mwisho na kuangalia hali ya mapato ya mume na halafu kutengeneza mipango ya ulipaji.

   31. Iwapo baba atamwita binti yake arudi nyumbani kwa sababu mumewe hajamaliza kulipa sehemu ya mahari, basi baba huyo anavunja sheria na anastahili kutozwa faini isiyopungua shilingi 100/-.

   32. Mume na mke wana uhuru wa kuhamia po pote hata kama mahari hayajalipwa yote.

   33. Kama mume akifa kabla hajamaliza kulipa mahari yote, ndugu yule aliyekubaliwa na mjane kuishi naye kama mume wake ndiye atakayemaliza kulipa sehemu iliyobaki.

Kugawanywa kwa Mahari

   34. Makabila mengine hayana kawaida ya kugawanya mahari kati ya jamaa wa kuumeni na wa kikeni.

   35. Makabila mengine yana tabia ya kumwachia baba wa binti kugawanya sehemu za mahari. Kiasi cha mafungu ni kama inavyokubaliwa kati ya baba na ndugu.

   36. Ndugu wanaopokea mafungu yo yote wana wajibu wa kuyarudisha kama ndoa ikivunjika na mahari ikibidi kurudishwa.

Urudishaji wa Mahari - Sheria za Kawaida

   37. A. Baba wa binti au mrithi wake anaweza kutakiwa kurudisha mahari wakati ndoa inapovunjika.

   B. Mtu anayeweza kudaiwa kurudisha mahari ni yule aliyepokea mahari au mrithi wake.

   38. Kiasi cha mahari kinachobidi kurudishwa na njia za kurudishia huamliwa na baraza.

   39. Urudishaji wa mahari yenyewe ni lazima ufanyike mbele ya mashahidi zaidi ya mmoja kutoka kila upande. Mashahidi ni lazima wafuatane na baba mkwe na mume au mawakili wao wa halali huko barazani ili washuhudie kiasi cha mahari kinachorudishwa.

   40. Deni la urudishaji wa mahari ni deni lililo muhimu kwa baba mkwe na uvunjaji wa sharti hili waweza kufikishwa mbele ya baraza la wenyeji kama kesi ya madawa.

   41. Kama mahari ikiwa na mifugo mume anaweza kudai kwamba wanyama wale wale aliowatoa ndio warudishwe iwapo bado wamo mikononi mwa baba mkwe. Hali kadhalika baba mkwe anaweza kurudisha wanyama wale wale aliopokea, na mume ni lazima awapokee hata kama hali yao imekuwa dhaifu.

   42. Iwapo baba mkwe hana hata mnyama mmoja kati ya wale waliolipwa kwa mahari, si lazima kwake kurudisha wanyama wa hali ile ile. Muda ambao mume na mke wameishi pamoja ni lazima ufikiriwe, lakini mume anaweza kukataa kupokea wanyama ambao hawana faida yoyote.

   43. Kama mume akikataa kupokea ng'ombe wa mahari ambao ni haki yake, na kama baraza likikata shauri kwamba ukatazi wake si wa haki, basi baraza linaweza kutoa talaka papo hapo.

   44. Mume hawezi kudai kwamba mahari aliyolipa irudishwe kwa kutoa vitu vile vile alivyotoa, isipokuwa kama vitu hivyo vimo mikononi mwa baba mke.

   45. Watoto wa wanyama waliolipwa kwa mahari, kama wanyama hao walikuwa ng'ombe au mbuzi, wasirudishwe. Vivyo hivyo kama mahari yalilipwa kwa pesa haitawezekana kudai faida ya pesa hizo.

   46. Kama ndama ambaye hajaacha kunyonya ikibidi arudishwe na mama yake, basi huhesabiwa kama ni mmoja wa wale wanaorudishwa.

Urudishaji wa Mahari baada ya Kufariki kwa Baba Mke

   47. I. Nyumba ya mke mmoja

   A. Baba ya binti akifa mrithi wake mkubwa ndiye atakayerudisha mahari.

   B. Kama baba hakuacha watoto wa kiume na mabinti wake ndio waliorithi mali yake, ambalyo pia ina mahari zao, basi mume anaweza kudai mahari toka kwa binti mkubwa wa marehemu.

   C. Kama mahari imepokelewa na rafiki akiwa kama mdhamini wa mke, yule mke ni wajibu wake kurudisha (tazama kifungu cha 24).

II   Nyumba yenye wake waliopalikwa.

   A. Mume ni lazima adai mahari kutoka katika nyumba iliyopokea mahari yake.

   B. Kama baba mkwe mwenyewe ndiye aliyepokea mahari hiyo wakati akiwa hai ni mrithi wake ndiye mwenye wajibu wa iuyarudisha bila kujali ni nyumba ipi alikotoka yule mke.

Urudishaji wa Mahari iwapo yule Binti anaolewa mara nyingine

   48. Kama baba mkwe hajamaliza urudishaji baada ya binti wake kuachika, ni lazima alipe deni lake mara tu akipokea mahari nyingine kwa ajili ya arusi ya pili.

   49. Ni lazima ikubaliwe kwamba wanyama na/au mali nyingine yoyote ya mahari ya mara ya pili ipelekwe barazani na wala sio nyumbani mwa baba mke. Mume wake wa kwanza au mdhamini wake ni lazima aitwe barazani siku ile ile ili apewe haki yake mbele ya baba mkwe.

   50. Kama kiasi kilicopo hakitoshikulipa deni lote, kile kiasi kinachobaki kinakuwa ni deni la muhimu, lakini mke ni lazima apewe talaka yake (tazama kifungu cha 59).

   51. Kama baba mkwe hafuati utaratibu wa kifungu cha 49 basi anaweza kuwa na hatia ya kulipa faini kiasi kisichopungua shilingi 100/-.

Urudishaji wa Mahari kama Ndoa ikivunjika

   52. Ndoa inapovunjika bila ya kutoka sababu maalum kwa mke au mume:

   A. Kama hawakuzaa, maisha ya ndoa tu ndiyo yafikiriwe katika kuweka kiasi cha mahari ambayo itarudishwa.

   B. Kama walizaa watoto, wawe wawili wanatoa sababu za kautaka kuachana, basi ni juu ya baraza kufikiri ni yupi aliye na makosa kati ya mke na mume au yupi kati yao ndiye chanzo cha kuvunjika ndoa.

   53. Wakati inapotokea kwamba mmoja au wote wawili wanatoa sababu za kutaka kuachana, basi ni juu ya baraza kufikir ni yupi aliye na makosa kati ya mke na mume au yupi kati yao ndiye chanzo cha kuvunjika ndoa.

   54. Ni uwezo wa baraza kubadili masharti yaliyomo katika kifungu cha 52 A na B na kufikiria kiasi cha mahari kinacobidi kurudishwa, nayo ni lazima ifuate kosa lenyewe.

   55. Baraza linapochungua juu ya shauri hili pia huchungua maisha ya ndoa.

   56. Kama mume ndiye mwenye makosa yule mke anapewa talaka mara tu baada ya baraza kukata shauri. Habari ya urudishaji wa mahari hufikiriwa pekee.

   57. Kama mume alimtesa mke wake kwa makusudi ya kupata chokochoko ya kuachana, basi baraza linaweza kuamua kwamba sehemu tu au chochote kisilipwe hata kama hawakupata mtoto.

   58. Kama mke ndiye mwenye makosa, hawezi kupewa talaka mpaka baba yake amalize kurudisha mahari yote au kama hana vifaa vya kumwezesha kufanya kama alivyoamriwa na baraza mara moja, basi kiasi kinachobaki kinakuwa kama deni la muhimu kwa yule baba.

   59. Kama mke mara kwa mara anafanya matendo mabaya ambayo mume yanamuudhi sana, hasa inapokuwa ni namna ya kumuudhi ili aweze kumwacha, baraza litashauri kwamba mahari yote au sehemu tu inabidi kurudishwa, hata kama mke na mume walipata watoto. Kama mume alikuwa hajamaliza kulipa mahari yote, baraza ni lazima lipime na likadirie hesabu ya malipo ya mahari yote kama ilivyokubaliwa na baba mkwe na bwana arusi.

   60. Wakati mmojawapo anang'ang'ania kuachana bila ya kutoa sababu yeyote, ni yeye ndiye atakayedhaniwa kuwa mwenye makosa.

   61. Upande ule ulio na makosa ndio hauna budi kulipa gharama zote za baraza na gharama ya hati ya Talaka.

Kama Mjane akirudi Kwao

   62. Mjane huulizwa kama anapenda kuchukuliwa na ndugu wa marehemu. Kama kikataa, mahari hairudishwei naye (mjane) ana uhuru kwenda kuishi na ndugu zake.

   63. Mjane ni lazima apewe hati ya kuthibitisha ujane wake na kwamba ametengana kabisa na jamaa ya marehemu mume wake.

   64. Kama mjane anakubali kuishi kama mke wa mmoja wa ndugu wa marehemu, na shauri likikubaliwa na baraza la ukoo, basi anakuwa mke halai wa ndugu hule.

   65. Mahari yale yaliyolipwa na marehemu hufikiriwa kama kwamba yamelipwa na ndugu yule.

Mjane mwenye Watoto walio hai au Waliokufa

   66. A. Mjane anayo haki ya kumchagua ndugu mmoja wa marehemu na kuishi naye kama mume wake, au anaweza kudai kuishi na watoto wake katika nyumba ya marehemu na atakuwa mmojawapo katika jamaa ya marehemu.

   B. Hata hivyo apewe hati ya kuthibitisha kuwa yeye ni mjane. (Tazama kifungu cha 63).

   67. Ingawaje mjane wa namna hiyo anatazamiwa kuishi na watoto wake tu, lakini hakuna ndugu aliye na haki ya kumfumania.

   68. Iwapo mjane kwa ung'ang'anizi wake anishi na mtu ambaye si ndugu ya jamaa wa marehemu, baraza la ukoo lina haki ya kumwonya na kama halikufaulu linaweza kumridisha kwa baba zake na pia kumnyang'anya watoto wake.

   69. Kama mjane akibeba mimba ya mtu ambaye si ndugu wa marehemu baraza la ukoo linaweza kuchagua ama kumrudisha yule mjane kwa baba zake au kumkubali mtoto atakayezaliwa kuwa ni mmoja katika watoto wa marehemu.

   70. Kama baba wa yule mtoto ni ndugu ya marehemu, basi mtoto siku zote hukubaliwa kuwa ni mmoja wa jamaa hiyo.

A. Matunzo kwa Mke aliyepewa Talaka

   71. A. Mke aliyekuwa wa Mkulima

   Atapata arobo ya mazao ya mwaka au ya daima, yaliyomo ghalani na makondeni katika mwaka ule ambao talaka imetolewa.

   B. Mke aliyekuwa wa mchuuzi, au wa mtuanayejitegemea.

   Atapokea fedha isiyopungua shilingi 150/- mara moja. Na kwa kufuata ukubwa na ushamivi wa kazi ya mume, itakuwa ni juu ya baraza kuongeza zaidi ya kima hicho.

   C. Mke aliyekuwa wa Mkulima ambaye pia ni Mchuuzi.

   Atapata kiasi kama kilichoelezwa katika kifungu cha 71.

   D. Mke aliyekuwa wa Mtumishi apokeaye mshahara daima.

   Atapokea mshahara wa mwezi mmoja wa mume wake.

   72. Malipo yaliyotajwa hapo juu yanaweza kufuatwa wakati mume anapopatikana na hatia peke yake mbele ya baraza, laiti kama mume siye mwenye makosa pekee, basi baraza linaweza kubadili malipo hayo kadiri ifaavyo. Ili kuepikana na shida katika kulipa, baraza litatengeneza tarehe na sehemu ya malipo ambayo mume itambidi kulipa.

   73. Kama mtalaka aliolewa tena, sehemu yeyote ambayo haijalipwa itafutwa.

   74. Kama mke ndiye mwenye hatia, mume hana lazima ya kulipa cho chote.

   75. Kwa kufuata masharti ya kifungu cha 71a, b, c, d yanamhusu hata mwanamke anayefanya kazi na kupata mshahara vile vile, isipokuwa kama maafikiano maalum yamefanywa na pande zote mbili.

   76. Katika hali zote za kuachana mke anachukua vitu vyake vyote, kama vile vitu alivyotoka navyo kwao, vitu alivyorithi, zawadi alizopewa na mumewe, zawadi toka kwa marafiti na kutoka kwa ndugu zake au ndugu wa mume wake.

B. Matunzo kwa Mjane Mgumba

   77. 1. Vitu vyaote vinavyoweza kuchukulika na visivyoweza kuchukulika ambazo vilichumwa wakati wa maisha ya ndoa vitagawanywa katika sehemu mbili sawa sawa baada ya kulipa madeni yote ya marehemu. Mjane atapata sehemu moja ya ishirini ya nusu moja kwa kila mwaka tangu waoane. Kwa vile vitu visivyochukulika mjane atapata sehemu ya ardhi kwa kufuata masharti kama yale yale na atakuwa na haki ya kutumia shamba kwa njuia bora wakati wote mapaka aoelwe tena au kufa kwake.

   2. Kwa mazao ya daima, atapata sehemu yake kwa masharti yale yale na ataweza kupata faida yake mpaka aoelwe au afe.

   3. Mjane aruhusiwe kukaa katika nyumba mpaka aolewe au afe.

   4. Mali yote isiyochukulika itarudi mikononi mwa ndugu wa marehemu mara tu baada ya mjane kuolewa au kufa.

   78. Kama mapato ya marehemu yalitokana na biashara au shughuli nyingine ambazo si za ukulima, baraza litakisia thamani ya mali, na mjane atapata fungu lake si za ukulima, baraza litakisia thamani ya mali, na mjane atapata fungu lake kama ihusikanavyo. Ni azi ya baraza kukata shauri juu ya ulipaji wa fungu hilo.

Kama Mke au Mume Akiugua

   79. Si mke wala si mume anaweza kumuacha mwenzake kwa sababu ya maradhi ya namna yo yote.

Juu ya Kifo

   80. A. Mahari haiwezi kurudishwa hata kama mke amezaa au hakuzaa.

   B. Kama mahari haikulipwa yote, mume hana lazima ya kumaliza.

   81. Sababu ya kifo haitazamiwi hata kama amejiua mwenyewe. Na wala muda tangu kuoana haufikiriwi.

   82. Kama mwanamke anafia katika nyumba ya mwanamume aliyekaa naye kinyumba. lakini ambaye ameanza kulipa mahari, sharti la kifungu cha 80B lifuatwe.

Kama Uchumba Umevunjika

   83. Kama uchumba umevunjwa na mmoja kati yao au kama mmoja wao akifa, ile sehemu iliyolipwa kwa ajili ya mahari ni lazima irudishwe, na kama ni mifugo basi inarudishwa pamoja na watoto.

   84. Kama mwanamke ndiye anayevunja uchumba basi inambidi kurudisha zawadi zote alizopokea toka kwa mchumba wake.

   Lakini kama ni mifugo basi inarudishwa pamoja na watoto.

Kikomo cha kuweka Madai kwa ajili ya kurudisha Mahari

   85. Baada ya kuthibitishwa kuachana na jinsi ya kurudisha mahari ikisha amuliwa, mume ni lazima akate shauri kabla ya mwezi mmoja kumalizika kama atapokea yale malipo au basi atasamehe. kama atasamehe basi mke lazima apewe hati ya talaka yake mara moja.

MLANGO WA PILI

Ushirika wa Kawaida 1, 2

(Ndoa)

   86A. Kama ndoa ni matokeo kati ya mapatano ya baba mkwe na mume, au ni matokeo ya mapatano ya watu wawili wanaohusika ni lazima ihalalishwe kwa kupatikana kwa cheti cha Ndoa. Zile desturi za kiasili ambazo hapo kale zilikuwa zikihalalisha ndoa hizo zinaweza kuendelea lakini hazihalalishi ndoa.

   B. Habari zote za ndoa ni lazima zipelekwe mbele ya baraza la Kienyeji lililopo karibu na nyumbani kwa yule mwanamke na kama huyo binti hakai na wazazi wake basi habari hizo zipelekwe kwenye baraza lililopo karibu ya kwao na mume.

   C. Watu wafuatao pamoja na maarusi watatakiwa kuhudhuria barazani kushuhudia ndoa:

   (a)   Baba wa bibi arusi au mbadala wake iwapo yule bibi arusi hajafikia umri wa miaka 21 (tazama vifungu 3 na 4).

   (b)   Shahidi mmoja anayejitegemea toka kila upande.

   87. Ada ya kuandikisha barazani na utoaji wa hati za ndoa ni lazima iwekwe kwa nchi nzima.

   88. Kama mjane anaolewa na ndugu ya marehemu ile ile hati ya kwanza inatosha lakini jina la yule ndugu ni lazima litiwe badala ya marehemu (tazama kifungu 65).

Kinyumba

   89. Kama mwanamume anamshawishi msichana aliye chini ya miaka 21 (aliye chini ya ulezi wa baba yake) ahame kwao na kukaa naye kinyumba, ana hatia na anastahili kulipa faini isiyopungua shilingi 50/- na kumlipa fidia baba wa yule binti isiyopungua shilingi 100/-. Fidia ni lazima ilipwe kabla ya faini.

   90. Mwanamume anayemtorosha mwanamke mara mbili tu kwa ajili ya kumtorosha binti yake.

   91. Faini na fidia haviwezi kuhesabiwa kama sehemu ya mahari iwapo mazungumzo juu ya ndoa yataanzishwa.

   92. Baba wa binti anaweza kumshtaki mwanamume mara mbili tu kwa ajili ya kumtorosha binti yake.

   93. Mali ya Bibi na Bwana ambayo wamekuwa wakikaa kinyumba inagawanywa kama ifuatavyo iwapo wamekata shauri la kutengana.

   94. Kama mwanamume na mwanamke wameshirikiana kuanzisha mahala pa maisha yao, vifaa vilivyopatikana kwa kushirikiana hugawanywa hivi:–

   Ng'ombe, vyakula vilivyomo ghalani, mazao ya kuuza, mazao ambayo hayajavunjwa, yanagawanywa sawa sawa kwa hao watu wawili. Nyumba hupewa mwanamume na mwanamke huchukua vyombo vya jikoni. Kila mtu huchukua vitu vyake vinavyohusu kama vile nguo mapambo n.k. pamoja na zawadi alizopokea toka kwa mwenziwe. Baada ya mavuno shamba ni mali ya Bwana.

   95. Kama mwanamke amemfuata mwanamume katika nyumba yake na kustarehe pale na kama wote wawili wameshirikiana kuendesha kazi kiwanjani mwao ama kama wote walikuwa na kazi maalum, mwanamke ana haki ya kupata robo ya vitu vyote vilivyopatikana kwa msaada wake isipokuwa vitu vyake mwenyewe kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 94.

   96. Kama bwana amefuata mwanamke mahala pake ana haki ya kupata robo ya vitu vyote vilivyopatikana kwa msaada wake isipokuwa vitu vyake kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 94.

   97. Kama mwanamke na mwanamume hawataki kufuata sharti lolote katika kifungu cha 94-95, ni lazima wafanye mipango wakati unaofaa. Kama hakuna mpango wowote uliofanywa, baraza lifuate mafungu 94-96.

MLANGO WA TATU

Kuachana (Talaka)

Sheria za kawaida

   98. A. Watu wanaweza kuachana pasi na kufika barazani bali kwa kufika barazani mwa maamuzi.

   B. Kwa hukumu ya baraza inayofuata mashtaka ya mume au mke.

   99. A. Utengenezaji wa baraza la maamuzi ni kazi ya sehemu hizi mbili ambazo zimekwenda sheriani.

   B. Kwa hukumu ya baraza inayofuata mashtaka ya mume au mke.

   C. Kama pande zote mbili zimekubaliana na hukumu ya baraza la maamuzi na baadaye upande mmoja hautimizi masharti yake, barza halina uwezo wa kulazimisha ile hukumu.

   D. Upande wenye hatia uanweza kushitakiwa na ule upande mwingine mbele ya baraza la wenyeji na wale maamuzi wakaitwa kama mashahidi kwa hukumu ya baraza lao.

   E. Waamuzi hawa hawana ruhusa ya kutoza faini au kudai ada; wanaweza kupokea zawadi ambazo ni lazima ziwe zimetolewa na pande zote mbili, kila upande ukilipa kama mwingine.

   100. Kama mume au mke akipatwa na ugonjwa wakati wa kusubiri shauri kuendeshwa, hukumu yoyote haitatolewa smpaka yule aliyeugua apate nafuu.

   101. A. Ni jambo la lazima kwamba mume na mke wakate hati ya kuachana hata kama kesi lilimalizika kwenye baraza la maamuzi au kwenye baraza la wenyeji.

   B. Daftari la talaka liwekwe katika kila baraza la wenyeji.

   C. Mke anafikiriwa ameolewa mpaka apate hati yake ya kuachana. Kabla kesi yake ya kuachana haijamalizika, yeye akingali ameolewa.

   102. Shauri likikatwa kwamba mahari lazima irudishwe basi ni lazima iandikwe ndani ya daftari la baraza, na kama mahari itarudishwa kwa vifungu vifungu, basi kila kifungu kiandikwe katika hati na kwenye daftari.

   103. Ada ya uandikishaji barazani na utoaji wa Hati za kuachana ni lazima iwekwe kwa nchi nzima.

   104. Watoto ni mali ya baba, naye ana haki ya kung'ang'ania kwamba aisi nao au waisi na ndugu zake. Mama naye ana haki ya kuwatembelea watoto wake mara kwa mara.

   105. Mtoto mchanga anabaki na mama yake mpaka ameacha ziwa kabisa, lakini gharama zo zote zinazohusu matunzaji ya mtoto ni juu ya baba yake.

Ugoni-Sheria za Kawaida

   106. Ugoni wa mke ni sababu kwa talaka.

   107. Mume anaweza kudai alipwe fidia kila anapomfumania mke wake, isipokuwa wakati baraza linapoona kwamba mume alikubali mkewe afanye zinaaa ili amfumanie na kuweza kulipwa fidia; katika hali kama hii yule aliyefumaniwa anaweza kusamehewa na baraza.

   108. Mashtaka yo yote ya uzinzi au madai ya fidia hayawezi kutiliwa nguvu mpaka uwepo ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba matendo ya uzinifu kati ya mke na mwanamume yametendeka.

   109. Ule ulipaji wa fidia haumpi haki yule mwanamume aliyefumaniwa ya kuchukua mtoto aliyezaliwa kama matokeo ya matendo yao.

   110. Kama mume anakaa nyumbani, ni yeye tu anayeweza kumfumania mkewe, isipokuwa anapokuwa mgonjwa, anaweza kutuma ye yote amtakaye akafanye hivyo kwa badala yake. Ni yeye tu anayeweza kudai fidia na.au kutoa talaka kwa mke wake.

   111. Kama mume hayupo nduguye wa kiume aliye karibu anaweza kumfumania yule mke, na kama mume hana ndugu wa kiume basi yule mtu aliyemchagua kumtunza mkewe kabla ya kuondoka ndiye mwenye mamlaka. Hao wenye mamlaka wanayo haki ya kudai fidia kwa badala ya mume ambaye hayupo.

   112. Ni mume tu anayeweza kukata shauri la kuachana au hapana.

   113. Baraza lina haki ya kukataa kusikiliza mashtaka ya ugoni ambayo bila sababu ye yote yamecheleweshwa na mshtaki baada ya kupata habari kamili juu ya jambo hilo. Kama mume hana habari yo yote juu ya ukweli mpaka anapoipata mara tu kabla au baada ya kuzaliwa mtoto, madai ya fidia hayawezi kufikiriwa kama yamecheleweshwa.

   114. Kama mgoni hatambuliki, lakini kama kuna uahkikisho juu ya tendo la uzinzi, mashtaka juu ya kuachana yanaweza kufikishwa barazani.

Kima cha Fidia na Faini

   115. A. Mtu anayepatikana na hatia ya ugoni ni lazima alipe faini isiyopungua dhilingi 50/- na alipe fidia kwa mume isiyopungua shilingi 100/-. Kima halisi cha fidia kitawekwa na baraza likifikiria hali ya kesi yenyewe. Mgoni ni lazima kwamza alipe fidia halafu ndipo alipe faini.

   B. Mke inambidi alipe faini isiyozidi shilingi 25/- isipokuwa kama ana mali yake mwenyewe na akionekana ana hatia zaidi kuliko mwenzake hapo baraza linaweza kumtoza faini kubwa zaidi.

BAYANA YA UGONI: USHAHIDI WA NAMNA MBILI UNAKUBALIWA KATIKA KESI ZA UGONI

A. Ushahidi ulio wazi

   116. Mume au mbadala wake (tazama kifungu 111) ni lazima awe na mashahidi zaidi ya mmoja aili kuhakikisha ugoni wake.

   117. Mashahidi lazima kujitambulisha kwa wale walhalifu wakati wakiwakuta.

B. Ushahidi usio dhahiri

   118. Lazima baraza liachiwe kufikiri kama habari iletwary mbele yake ni ushahidi wa kutosha kwa uzinzi au kama inahitajiwa kutibitishwa zaidi.

   119. Kama taarifa iliyopatikana inaonekana haitoshi kuhakikisha ugoni, basi uthibitisho ni lazima uongezwe. kwa ajili hiyo matendo yote yanayoonyesha ugoni yajumlishwe, kwa mfano:–

   Kama vitu vya mgoni vikitolewa.

   Kama mke akikiri.

   Alama za mapigo maungoni mwa mgoni.

   Kama mek akiwa ameambukizwa na magonjwa ya kisonono au kaswende.

   120. Uhtibitisho mwingine hautakiwi kama taarifa iliyopatikana haina tafsiri nyingine isipokuwa ile ya ugoni.

   121. Kama mke na mume wote wanaugua kisonono au kaswende na kama hakuna uthabiti wa ugoni basi talaka haiwezi kutolewa kwa sababu ya kuambukizwa ugonjwa.

   122. Kama ugoni umehakikishwa, mashauri huahirishwa mpaka mwenye kuumia apone (kfingu cha 165).

   123. Mtu aliyemuabukiza mke wa mtu ni lazima alipe gharama zote zinazotokana na matatibu ya ugonjwa-mbali fidia na faini ya ugoni.

Ugoni wakati Mume ameondoka kwa muda mrefu

   124. Kama mume akirudi baada ya kuondoka kwa muda mrefu na akamkuta mke wake anakaa kinyumba na mtu mwingine, anaweza kudai kuachana na pia anaweza kudai fidia ya ugoni bila ya kuhitaji uhakikisho zaidi.

   125. Kama mume akirudi na kumkuta mke wake kabeba mimba au amezaa mtoto ambaye hawezi kuwa wake kwa sababu ya kutokuwako kwake, njia nyingi anaweza kuzifuata:

   A. Anaweza kudai fidia ya ugoni, akakataa kumpokea mtoto yule kama wake na kumsamehe mke wake; kwa hiyo yule mtoto anakuwa ni wa ujombani.

   B. Anaweza kudai fidia ya ugoni, kumkubali mtoto kuwa wake na kumsamehe mke wake.

   C. Anaweza kudai fidia ya ugoni akamwacha mke wake. Yule mtoto wa mgoni anakuwa ni wa ujombani.

   126. Mume akirudi hana budi kukata shauri mara moja juu ya mimba au juu ya mtoto yule wa mke wake. Ikiwa mume baada ya kurudi hakati shauri na anazidi kuendelea na maisha yake ya ndoa kama desturi, inafahamika kwamba amemsamehe mke wake na amekubali ubaba.

   127. Kama wakati mume anaporudi, anapata ushahidi kwamba mke wake amefanya zinaaa, au alikaa na matu mwingine wakati yeye alipokuwa hayupo, laini yule mke akavunja urafiki kabla mume wake kurudi, basi yule mume hawezi kudai fidia ila anaweza kudai kuachana.

   128. Kama muem akirudi na kupata habari kwamba mke wake alifia katika nyumba ya hawara yake, mume anaweza kudai arudishiwe mahari yote aliyolipa kwa kufuata kifungu cha 52. Katika hali kama hii yule hawara atalipa fidia na faini kama zilivyoelezwa katika kifungu cha 115.

Ugoni Utokeao kwa kutojali hali ya Mwanamke

   129. Ni wajibu wa mwanamume kupata hakika kwamba mwanamke anayetembea naye au anayemuoa hana mume. Usemi wo wote wa mwanamke hata kama akiutoa mbele ya mashahidi hauwezi kuwa ngao kama mwanamume akishtakiwa kwa ugoni.

   130. Kama mambo yaliyvo yakionyesha kwamba mwanamume ameshindwa kwa haki kutambua ukweli basi hawezi kushitakiwa kwa ugoni.

   Kwa mfano:

   Ikifika habari nyumbani kwamba mume amefia mahali mbali na kwao na ndugu zake wakafanya matanga kama kawaida. Mjane akiolewa na mume mwingine ambaye katoa mahari. Baadaye yule mume wa kwanza akitokea, basi ule uvumi wa kifo chake ulikuwa si wa kweli. Na kama hakuna ye yote kati ya waume hawa wawili aliye tayari kwa hiari yake kumwacha yule mwanamke, basi mke ataulizwa ni yupi anayempenda kuishi naye. Yule asiyechaguliwa hurudishiwa mahari yake, na kama alizaa nae, mtoto mmoja au zaidi, anaweza kuwachukua. Baraza linaweza kukata shauri kama sehemu ya mahari isirudishwe na ipokelewe na baba wa mke kwa malezi ya mtoto au watoto.

   131. Kama mwanamume akitambua kwamba kimada wake ni mke wa mtu mwingine, ni lazima afarakane naye mara moja. Kama akiendelea kukaa naye ingawa akienda kutoa habari kwa jumbe, basi atakuwa na hatia ya kulipa fidia kama atakutwa na mume wake akiishi na yule bibi.

   132. Kama mtu aliyeshikwa na mume katika matendo ya uzinifu akiweza kuhakikisha kwamba yule mwanamke ni malaya, basi mume hawezi kudai fidia, bali anaweza kumtaliki yule mwanamke.

Kuasi

   133. Kuasi kwa mke ni sababu inayoweza kuleta kuachana.

   134. Mume ana haki ya kudai kuachana na kutaka kutengenezwa mashauri ya mahari kwa mintarafu ya kifungu cha 54, kama anajua mahali gani mkewe anapokaa, au kama anaweza kuhakikisha kwa bayana au kwa dalili kwamba mkewe ameasi.

   135. Haifikiriwi kuwa ni uasi kama mke akimwacha mume wake na akaenda kwa jamaa yao.

   136. Kama mke akienda kwa jamaa kwanza, na baada ya kukaa huko kwa muda mfupi akahama na akienda kwingine tu, mume wake anaweza kumshitaki mkewe bila ya yeye kulazimika kutoa maelezo juu ya mahali alipo.

   137. Mtu ye yote anayemficha mke wa mtu na kukana kwamba hayumo nyumbani mwake wakati mumewe anapofika kumtafuta, ni lazima ampashe habari jumbe juu ya kuweko kwa bibi yule. Kama asipofanya hivyo anastahili kutozwa faini isiyozidi shilingi 50/-.

   138. Hitilafu yake ni ndugu ambaye hawezi kutozwa faini kwa sababu anaweza kuona huruma juu ya ndugu yake na kutaka kumponya iwapo akiona makusudio ya mume ni mabaya.

   139. A. Si ndugu wala si mtu ye yote aweza kulaumiwa au kuadhibiwa kwa kumkaribisha mwanamke nyumbani au kwa ktomwarifu mumewe (ikiwa anamjua) juu ya kuwasili kwa mke wake.

   B. Kama mtu anataka kujiepusha na hatari ya kutiwa katika kesi ya ugoni, basi ni lazima ampeleke mwanamke kwa jumbe au wa chini yake.

   140. Haifikiriwi kwamba ni wajibu katika sheria kwa mume kutafuta mke wake aliyemuasi.

   141. Mume ambaye mke wake alimuasi na akarejea baadaye, hawezi kudai fidia. kama akisikia kwamba mkewe alizini wakati alipokuwa hayuko kwake, anaweza kudai kuachana naye kama hataki kumpokea tena.

Kutoroshwa

   142. Kama mtu akimshawishi mke wa mtu, amwache mume wake na atoroke naye, mume anaweza kudai talaka.

   143. Kama hao wawili walikutwa mahala pengine wawe wanaishi nyumba moja au mbali mbali, hakuna haja ya kuhakikisha kwamba wamezini, kwani zinaa inafikiriwa kuwa imehakikishwa.

   144. Mwanamume na mwanamke waadhibiwe kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 115A na B. Zaidi ya hivyo mwanamume ni lazima alipe faini isiyopungua Shilingi 50/- na mwanamke ni lazima alipe faini isiyopungua Shilingi 25/-.

   145. Ukweli kwamba mke alimfuata hawara yake kwa hiari yake hauwafanyi wote wawili kutokuwamo hatiani.

   146. Mtu ye yote anayewakaribisha mwanamke na mwanamume ambao anajua kuwa wametoroshana anastahili kutozwa faini isyo chini ya Shilingi 50/-.

   147. Kama mke ametoroka na bwana, lakini haisi naye wakati mume wake anapomuona, bwana anayeishi naye ni lazima alipe ugoni. Kama mke haishi na bwana ye yote, basi yeye aliyemtorosha ndiye anayestahili kulipa ugoni.

Kukataa kumfuata mume

   148. Kama mke alikataa kufuatana na mumewe ambaye anakusudia kuhamia mahala pengine katika wilaya au nje ya wilaya yao, mume ana haki ya kudai kuachana na hukumu juu mahari ni juu ya baraza.

   149. Kama kuna watoto baba yao anaweza kuwachukua na kuenda nao hata kama hajamaliza kulipa mahari yote.

Madhara kutokana na mke

   150. Kama mwanamke akimpiga au kumuumiza mumewe, basi ni juu ya baraza kuamua kama tendo hilo ni sababu ya kuachana au kukataa. Kama bibi ana mali yake mwenyewe baraza linaweza kutoza malipo ya fidia, kwa kadri kama ilivyoonyesha katika kifungu cha 167A-C.

Dharau

   151. Kutoangalia kazi ya nyumbani siku zote, mambo ya kuabisha, utovu wa haya au tabia ya ulevi kwa mke hukubaliwa kuwa ni sabau ya kuachana.

   152. A. Kama ikihakikishwa kwamba mke amekunywa dawa ya kutoa mimba na akafanikiwa, mume ana haki ya kudai kuachana.

   B. Kama ikiwezekana kuhakikishwa kwamba mke amekunywa dawa na mganga, awe mwanamke au mwanamume, mganga anastahili kutozwa faini isiyopungua Shilingi 200/- ama kufungwa hivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha jinai.

   C. Kama mke anashindwa kuzaa hii sio sababu ya kuachana.

Ukatazi wa haki za mume na mkewe

   153. Kama mke akikataa kulala na mumewe mara kwa mara pasi na sababu yo yote inayohusikana na mwili wake, basi hali hiyo ni sababu ya kuachana.

   154. ganga ambaye alimuagua, au kumpa dawa za uchawi mke alikwenda kwa mganga kupata dawa za uchawi bila ya ruhusa ya mume wake, basi bwana anaweza kudai kuachana.

   155. Mganga ambaye alimuagua, au kumpa dawa za uchawi mke wa mtu bila idhini ya mumewe anastahili kutozwa faini isiyopungua Shilingi 100/-.

Utasa wa mke

   156. Utasa wa mke hauwezi kuwa sabau ya kuachana.

B. Mashtaka yaletwayo na mke-Ugoni

   157. A. Kwa kawaida za mila ugoni wa mume haufikiriwi sababu ya kuachana, lakini baraza linaweza kukata shauri ya kutoa talaka kwa sababu ya uzito wa kesi yenyewe.

   B. Mume akizini na binti yake au binti yake wa kambo ni sababu za kuachana.

   158. BAraza linaweza kuamuru kutokana na zinaa ya maharimu kwamba watoto wapewe ndugu wa mume kuwatunza. Kama hakuna ndugu wa mume basi ndugu wa mke anaweza kuteuliwa awe mtunzaji.

   159. Kwa hali yo yote ya manma hii watoto wanaendelea kushika kikao chao kwa kufuata masharti yanaohusu kawaida za kuumeni.

Kuasi

   160. A. Kama mume akiondoka nyumbani kwa muda zaidi ya mwaka mmoja na nusu mke wake anaweza kudai talaka. Sharti hili vile vile linahusu hata kama mume amekuwa akitoa matumizi na utunzaji wa mkewe au kama mume alimwacha mkewe katika uangalizi wa ndugu yake.

   B. Mume ambaye anakwenda fanya kazi nje ya Tanganyika kwa muda unaozidi mwaka mmoja na nusu na hawezi kuenda na mkewe, basi ni lazima afanye mipango maalum na mkewe kabla hajaondoka ili yule mke asiweze kutoa maombi kuhusiana na kifungu cha 160A.

   161. Kama mahala alipo mume panajulikana basi ni lazima aarifiwe na baraza kwamba mkewe atapewa talaka kama yeye hataki kurudi mapema.

   162. Kama baraza likiamua kuwa sehemu ya mahari iridushwe basi atapewa ndugu wa mume ambaye vile vile atawachukua watoto wa msafiri.

Madhara kutokana na mume

   163. Mabaraza yanafikiria madhara mabaya tu kuwa sababu ya kuachana. Madhara yafuatayo yanafikiriwa kuwa makubwa na kuleta kuachana na kuhusu kima cha mahari ambayo itarudishwa (tazama kifungu cha 54).

   Kwa mfano:

   Jeraha lolote liletwalo na kitu chenye makali, kuvunjika, kutia ulema wa daima, kuharibu sura kwa daima, kutenda maovu kwa kuendelea.

   164. Matendo ya nguvu yafuatayo na matokeo yao ya kawaida hayafikiriwi kuwa ni sabau za kuachana: Makofi au ngumi, kupiga kwa fimbo (hata kama kutia machubuko au uvimbe), kusukuma, kupiga mateke, kumtupia mke vitu vya nyumbani.

   165. Kesi inaahirishwa mpaka mke apone au mpaka hapo anapopata nafuuu ya kutosha.

   166. Mke ana haki ya kupata fidia kwa majeraha hata kama talaka inatolewa au hapana. Baraza linaweza zaidi ya kutoza fidia kwa mume vile vile kumfaini au kutoa hukumu ya kifungo.

   167. Kipimo cha fidia kinahitilafiana kwa kufuata ubaya wa madhara yaliyofanyika:

   A. Mapigano, michapo, kuvunjika kidole, kupoteza/kuvunjika jino, jeraha dogo dogo ambalo limepona kabisa-fidia yake si chini ya Shilingi 10/- wala haizidi Shilingi 100/-.

   B. Kupiga kwa mara kwa mara, kuvunja mguu au mkono ambao unaweza kuponeshwa-fidia yake si chini ya Shilingi 100/- na wala haizidi Shilingi 100/.

   C. Madhara ya daima kwenye jicho, kuharibu kiungo daima, kupoteza sehemu na nje ya sikio, kuharibu sura maisha-fidis yake si chini ya Shilingi 200/- na wala haizidi Shilingi 500/-.

   D. Inapotokea kuwa kilema ni kibaya sana baraza linaweza kutoa amri kwamba mume baada ya kumuacha mkewe anabaki na wajibu wa kumtunza yule bibi mpaka kufa kwake.

   Kumbuka: Kama mume akimtukana mkewe haifikiriwi kuwa ni sababu ya kuachana.

Kutojali wajibu wa mume na mke

   168. Kama mume akikataa kulala na mke wake kwa muda mrefu, baraza litachungua yote yanayohusika na kesi hiyo na kama baraza likiona kwamba kule kutojali kulikuwa kwa makusudi basi linaweza kutoa talaka.

Uhanithi

   169. Mke anaweza kupewa talaka kama ikihakikishwa:

   A. Kwamba mume alikuwa hanithi wakati wa arusi, yaani wakati ya usiku wa arusi na siku chache zifuatazo.

   B. Kwamba mume bila shaka amekuwa hanithi katika miaka mitano ya kwanza ya maisha ya ndoa.

   C. Kama bwana hana kizazi haiwezi kufikiriwa kuwa ni sababu ya kuachana.

Uzinfu usio wa kawaida

   170A. Desturi chafu zinazochikiza, kulawiti (kufira) au kitendo cho chote cha uzinifu usio wa kawaida zinakubaliwa kuwa ni sababu za kuachana.

   B. Kumwaga mbegu upesi sana wakati wa kulalana inafikiriwa kuwa ni sababu ya kuachana.

Kutojali utunzaji

   171. Makusudio wazi ya kutojali watu wa nyumbani mwake pamoja na matendo mabaya nafikiriwa kuwa ni sababu za kuachana. mambo madogo madogo kama vile kushindwa kupata nguo, vitu vya kike au kitoweo hazifikiriwi kuwa ni sababu za kuachana.

   172. Kama kuachana kunatokea kwa sababu ya kutojali jamaa kabisa, baraza lina haki ya kuweka masharti juu ya uangalizi wa watoto, lakini baba hawezi kunyimwa watoto wake, lakini anaweza kunyang'anywa asiwalee.

Kutopatana

   173. Kama wote mke na mume wanang'ang'ania kuachana bila ya kutoa sababu yo yote, basi talaka itatolewa lakini masharti ya kifungu cha 52 yatafuatwa.

   174. Kama mmoja tu kati ya wawili ndiye anayeng'ang'ania kuachana bila ya kutoa sababu za kuachana basi talaka itatolewa lakini madai hayo yasiokuwa na sababu yatafikiriwa kuwa ni kosa upande wa mng'ang'anizi na kifungu cha 54 kitafuatwa.

MLANGO WA NNE

Hali ya Watoto

1. Watoto wa halali

   175. Watoto wasiozaliwa katika hali ya ndoa ni mali ya jamaa ya kukeni, yaani ni mali ya baba ya mama yao.

11. Watoto wa kambo

   176. Kama mtoto anaishi na mama yake katika nyumba ya baba yake wa kambo hawezi kabisa kuwa kwa sheria mmoja wa jamaa ya baba ya kambo.

   177. Kama baba baada ya upata watoto na mkewe wa kwanza akamwacha na kuoa mke mwingine, watoto hawa wa kwanza wanashikilia cheo chao hata kama mama wa kambo akizaa.

111. Watoto wasio halisi

A. Kama baba hajulikani

   178. Watoto wasiozaliwa katika hali ya ndoa ni mali ya jamaa ya kukeni, yaani ni mali ya baba ya mama yao.

   179. Kama baba ya mama ana watoto wa kiume basi huyu naye anafuata nyuma ya wale katika jamaa.

   180. A. Kama mtoto ni msichana, basi mahari yake hupokelewa na babu yake mzaa mama au mrithi wake.

   B. Kama babu hana watoto basi huyu mtoto asiye halisi anakuwa kama mtoto wake wa halali.

B. Kama baba anajulikana: Kuhalalisha

   181. A. Baba ana haki ya kuhalalisha watoto wake wasio halisi wakati wo wote kwa kumuoa mama yao.

   B. Kama matu akitaka kumhalalisha mtoto wake bila ya kumwoa mama yake anaweza kufanya hivyo kwa kulipa fidia Shilingi 100/- kwa baba ya msichana kabla mtoto hajaacha ziwa.

   C. Mahala atakapoishi mtoto patakubaliwa na baba na mama wa mtoto au wakishindwa kukubaliana basi patawekwa kwa amri ya baraza. Kwa hali yo yote baba atakuwa na wajibu wa kumtunza mtoto.

   182. Ni mtu yele pake yake ambaye alitajwa na mama wakati wa kuzaa kuwa ndiye baba wa mtoto, ndiye mwenye haki ya kumhalalisha mtoto.

   183. Mwanamume ambaye ametajwa na mwanamke kuwa ndiye baba wa mtoto hana budi kumkubali kwamba yeye ndiye baba wa mtoto ila akiweza kuhakikisha kwamba hakuzini na yule mwanamke.

   184. Hata kama mwanamke alikuwa akitembea na mabwana zaidi ya mmoja, wakati alipopata mimba, yule ambaye atatajwa na mwanamke huyo, hawezi kukataa kuwa baba wa mtoto huyo.

   185. Muda ambao mimba ingaliweza kuingia unafikiriwa kutimiza miezi miwili, yaani miezi saba kabla ya uzazi.

   186. Kama mwanamume aliyetajwa akishikilia kukana kwamba hakupata kuzini na yule mwanamke na akileta ushahidi, basi mwanamke atatakiwa uthabiti wa madai yake kwa kutoa maelezo kamili juu ya mahala na wakati, kueleza maumbo ya mwanamume na kwa kuita mashahidi wanaojua kuhusiana kwa mwanamke na mwanamume huyo.

   187. Kama mwanamke akimtaja mtu aliyemtia mimba naye na yeye anahakikisha kuwa maneno hayo ni ya uwongo, madai ya ubaba yatafutwa, hapo mwanamke hataruhusiwa tena kutaja mwanamume mwingine.

   188. Kama mwanamke anaishi kinyumba na mwanamume, basi huyo bwana ndiye mwenye mimba hiyo. Kama yule bwana akitaka kukataa juu ya kuhusikana na mimba hiyo basi ni juu yake kuhakikisha madai yake.

   189. Mtu aliyetia mimba ana wajibu wa gharama zote za mimba na za kuzaliwa kwa mtoto.

Faini na fidia inayohusu mimba isiyo halisi

   190. Mwanamume ambaye anahusika na kumtia mimba mwanamke aliye chini ya umri wa miaka 21 anastahili kulipa faini isiyopungua Shilingi 80/- na kulipa fidia isiyopungua Shilling 100/- kwa baba wa binti huyo.

   191. Faini alipwe baada ya mashauri ya baba wa mtoto kumalizika na fidia ilipwe baada ya mtoto kuzaliwa.

   192. Ni wajibu wa baba wa mtoto na baba wa mama mtoto kuafikiana juu ya arusi na juu ya uhalali wa yule mtoto. Bidii zote lazima zifanywe kumshawishi baba wa binti akubali juu ya ufungaji ndoa na juu ya mahari, kima chake kifuate mapato ya yule wana na juu ya malipo ambayo yatatolewa kabla ya kufunga ndoa na baada ya kufunga ndoa. (Tazama kifungu cha 10B).

   193. Ulipaji wa fidia haumpti haki yule bwana juu ya mtoto.

   194. Inapotokea kuwa mimba inaharibika malipo yote ya faini na fidia ni lazima yatimizwe kama dalili ya mimba ikihakikishwa.

   195. Kama baada ya mimba ya kwanza ndoa haikufungwa na halafu mwanamke akibeba tena mimba na kupata mtoto mara ya pili wa bwana yule yule, basi hakuna faini na fidia itakayolipwa.

   196. Kama bwana akimuoa mwanamke anapobeba mimba mara ya pili, basi kwa sababu hiyo yule mtoto wake wa kwanza pia anakuwa halali.

   197. Kama baba wa mwanamke alikubali kupokea mahari toka kwa bwana arusi wa binti yake na hivi akatoa idhini juu ya nadoa, yule bwana hana haja ya kulipa faini wala fidia.

   198. Kama mapacha yakizaliwa faini na fidia ilipwayo ni sawa na mtoto mmoja.

   199. Kama baba wa mtoto hana kitu, basi deni la fidia linakuwa muhimu.

SECOND SCHEDULE
MODIFICATIONS OF THE DECLARATION SET OUT IN THE FIRST SCHEDULE IN RELATION TO CERTAIN AREAS

   (a)   The area subject to the jurisdiction of the Buhaya District Council:

      Paragraph 125:

         Delete the full stop at the end of subparagraphs A and C and substitute the words and full stop: "au wa mgoni".

      Paragraph 170:

   (b)   The area subject to the jurisdiction of the Kwimba District Council:

      Paragraph 11:

         Delete the tale in subparagraph A and substitute the following table:–

         "Ng'ombe jike 1 kwa mbuzi 10 au kondoo 10

         Ng'ombe jike 1 kwa Shilingi 200/-

         Fahali 1 kwa Shilingi 100/-

         Mbuzi 1 kwa Shilingi 20/-

         Kondoo 1 kwa Shilingi 20/-".

   (c)   The area subject to the jurisdiction of the Ukerewe District Council:

      Paragraph 11:

         Delete the items:–

         "Ng'ombe jike 1 kwa mbuzi 5 au kondoo 5

         Ng'ombe jike 1 kwa Shilingi 100/-

         Fahali 1 kwa Shilingi 90/-"

         in subparagraph A and substitute the following new items:–

         "Ng'ombe jike 1 kwa mbuzi 10 au kondoo 10

         Ng'ombe jike 1 kwa Shilingi 200/-

         Fahali 1 kwa mbuzi 5 au kondoo 5

         Fahali 1 kwa Shilingi 100/-".

      Paragraph 170:

         Delete subparagraph B.

      Paragraph 181:

         Delete the full stop at the end of subparagraph B and substitute the words and full stop:

         "au kabla ya miaka miwili tangu kuzaliwa mtoto: muda unayozidi ufuatwe."

THE LOCAL CUSTOMARY LAW (DECLARATION) (No. 2) ORDER

[1st August, 1963]

G.N. No. 303 of 1963

   1. This Order may be cited as the Local Customary Law (Declaration) (No. 2) Order.

   2. The declaration set out in the First Schedule to the Local Customary Law (Declaration) Order, 1963, is hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained therein in the areas subject to the jurisdiction of the Dodoma, Iramba, Mpwapwa, Manyoni, Shinyanga, Singida and Ufipa District Councils.

THE LOCAL CUSTOMARY LAW (DECLARATION) (No. 3) ORDER

[1st August, 1963]

G.N. No. 380 of 1963

   1. This Order may be cited as the Local Customary Law (Declaration) (No. 3) Order, and shall come into force on the first day of September, 1963.

   2. The declaration set out in the First Schedule to the Local Customary Law (Declaration) Order, 1963 *, is hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained therein in the areas subject to the jurisdiction of the Kasulu, Kibondo and Kigoma District Councils.

   3. Subject to the respective modifications set out in the Schedule to this Order in relation to the areas of the several District Councils, the declaration set out in the First Schedule to the Local Customary Law (Declaration) Order, is hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained therein in the area subject to the jurisdiction of the Chunya, Geita, Mbeya and Tanga District Councils.

SCHEDULE
MODIFICATIONS OF THE DECLARATION SET OUT IN THE FIRST SCHEDULE TO THE LOCAL CUSTOMARY LAW (DECLARATION) ORDER, 1963, IN RELATION TO CERTAIN AREAS

   (a)   The area subject to the jurisdiction of the Chunya District Council:

      Paragraph 11:

         Delete the table in subparagraph A and substitute the following table:–

         "Ng'ombe jike 1 kwa shilingi 200/-

         Fahali 1 kwa shilingi 100/-

         Mbuzi 1 kwa shilingi 20/-

         Kondoo 1 kwa shilingi 20/-".

   (b)   The area subject to the jurisdiction of the Geita District Council:

      Paragraph 11:

         Delete the table in subparagraph A and substitute the following table:–

         "Ng'ombe jile 1 kwa mbuzi 10 au kondoo 10

         Ng'ombe jike 1 kwa shilingi 200/-

         Fahali 1 kwa shilingi 100/-

         Mbuzi 1 kwa shilingi 20/-

         Kondoo 1 kwa shilingi 20/-.".

      Paragraph 160:

         Insert after the word "nusu" in the first line of subparagraph A the words and brackets: "(ila akiwa hospitalini mgonjwa au kifungoni)"

   (c)   The area subject to the jurisdiction of the Mbeya District Council:

      Paragraph 11:

         Delete the table in subparagraph A and substitute the following table:-

         "Ng'ombe jike 1 kwa mbuzi 10 au kondoo 10

         Ng'ombe jile 1 kwa shilingi 200/-

         Fahali 1 kwa shilingi shilingi 150/-

         Mbuzi 1 kwa shilingi 20/-

         Kondoo 1 kwa shilingi 20/-.".

      Paragraph 160:

         Insert after the word "nusu" in the first line of subparagraph A the words and brackets:

         "ila akiwa hospitalini mgonjwa au kifungoni)".

   (c)   The area subject to the jurisdiction of the Mbeya District Council:

      Paragraph 11:

         Delete the table in subparagraph A and substitute the following table:–

         "Ng'ombe jike 1 kwa mbuzi 10 au kondoo 10

         Ng'ombe jike 1 kwa shilingi 200/-

         Fahali 1 kwa shilingi 150/-

         Mbuzi 1 kwa shilingi 20/-

         Kondoo 1 kwa shilingi 20/-.".

      Paragraph 155:

         Add the following words and fullstop:–

         "Mke aadhibiwe vile pia.".

   (d)   The area subject to the jurisdiction of the Tanga District Council:

      Paragraph 28:

         Add the following words and fullstop:–

         "Ikiwa mnyama amekufa, baba wa binti arusi ataleta ngozi na nyama kuwa ni uthbitisho maalum wa kifo cha mnyama aliyekufa.".

         ni uthibitisho maalum wa kifo cha mnyama aliyekufa.".

THE LOCAL CUSTOMARY LAW (DECLARATION) ORDER (1967)

(Section 9A (Sixth Schedule))

[1st July, 1967]

G.N. No. 219 of 1967

   1. This Order may be cited as the Local Customary Law (Declaration) Order.

   2. The declarations set out in the First, Second and Third Schedules to the Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order * are hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained thererin in the area subject to the jurisdiction of the Pangani District Council and to be binding upon Africans to whom the local customary law relates.

THE LOCAL CUSTOMARY LAW (DECLARATION) (No. 4) ORDER

[1st October, 1963]

G.Ns. Nos.
436 of 1967
219 of 1967

   1. This Order may be cited as the Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order.

   2. The declarations set out in the First, Second and Third Schedules to this Order are hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained therein in the areas subject to the jurisdiction of the Chunya, Dodoma, Kasulu, Kibondo, Kigoma, Kondoa Manyoni, Maswa, Mbeya, Mpwapwa, Ngara, Njombe, Shinyanga, Singida, Songea, Ufipa, Ukerewe and Pangani District Councils.

FIRST SCHEDULE
SHERIA ZA ULINZI

   (1) Ulinzi huwa wa namna hizi zifuatazo:

   (a)   ulinzi wa watoto waliofiwa na baba wakati wadogo;

   (b)   ulinzi wa mrithi ambaye hayupo wakati wa kurithi;

   (c)   ulinzi wa mtu ambaye hawezi kujitegemea kwa sababu ya umaskini au wazimu;

   (d)   ulinzi wa mke na mtoto wa mtu anayekwenda safari ndefu.

Ulinzi wa watoto:

   (2) Mlinzi wa watoto wadogo walifiwa na baba atawekwa na baraza la ukoo.

   (3) Ikiwa mtoto wa kiume wa kwanza ni mtu mzima, ndiye atakayewekwa kuwa mlinzi wa watoto wadogo wenzake akiwa yeye ni mwenye akilina ana tabia nzuri.

   (4) Ikiwa mtoto wa kiume wa kwanza hafai, atawekwa ndugu mwingine wa ukoo wa marehemu.

   (5) Kama baba aliyekufa alikuwa na wake wengi, kila mtoto wa kiume wa kwanza (akiwa ni mtu mzima na akifaa) toka kila nyumba, atafikiriwa kwanza kuwa mlinzi wa wadogo zake katika nyumba yake.

   (6) Mlinzi anapowekwa huelezwa na baraza la ukoo wajibu wake wa ulinzi. Kama hakuelezwa, ni juu yake kupata maelezo ya wajibu wake toka baraza la ukoo.

   (7) Mama mjane akikubali kurithiwa na ndugu mmoja wa marehemu na amekubaliwa na baraza la ukoo, yeye ndugu ndiye atakayekuwa mlinzi wa watoto wa marehemu.

   (8) Ikiwa mlinzi hatimizi wajibu wake, baraza la ukoo lina uwezo wa kumwondoa na kuweka mwingine badala yake, kwa kufuata madai ya mama au ya ndugu yeyote wa ukoo wa kiume.

   (9) Mlinzi hawezi kuuza ardhi wala mimea ya daima iliyo chini ya ulinzi wake.

   (10) Mlinzi hapati mshahara au malipo maalum kwa kazi yake ya ulinzi, lakini kwa kawaida hukaribishwa kwa vyakula na vinywaji.

   (11) Kazi ya mlinzi ni kuwatunza watoto na mama yao, na kuangalia mali yao isipotee wala isiharibike.

   (12) Mlinzi ana wajibu wa kuongoza kazi ya kilimo, lakini ashauriane na mama ikiwa yupo nyumbani kwa watoto.

   (13) Mlinzi anaweza kumwoza mtoto wa kike, lakini katika shauri hili kwanza akubaliane na mama.

   (14) Mlinzi atashughulika na mambo yote ya nje yanayohusu nyumba ile, kwa mfano: kusimamia mashauri, malipo ya kodi na ushuru, ada ya shule, kuhudhuria minada ya mifugo, n.k.

   (15) Mlinzi ana wajibu kuangalia mali ya watoto walio chini ya ulinzi wake, bila kuichanganya na mali yake: yaani, mali ya watoto lazima yajulikane kwazi.

   (16) Mazao ya mashambani yatatumika nyumbani kwa manufaa ya watu wa nyumbani.

   (17) Mazao ya mifugo kama maziwa na samli yatatumika vile vile nyumbani kwa manufaa ya watu wa nyumbani.

   (18) Wanyama watakaozaliwa na mifugo pia ni mali ya watoto.

   (19) Mlinzi anaweza kuchinja, kuuza au kubadilisha wanyama kwa faida au mahitaji ya nyumbani.

   (20) Kama marehemu alikuwa na wake wawili au zaidi, na hakuna mjane aliyekubali kurithiwa, baraza la ukoo linaweza kuweka mlinzi mmoja kwa nyumba zote.

   (21) Mashtaka au madai juu ya ulinzi yanaweza kuletwa na mama wa watoto, ndugu mwingine, na hata na watoto wenyewe watakapokua.

   (22) Mashauri kama haya yasipokelewe na baraza la hakimu ikiwa hayakufikishwa kwanza kwa baraza la ukoo.

   (23) Mlinzi akifa, atawekwa mwingine na baraza la ukoo.

   (24) Mrithi wa kwanza atakapofikia umri wa miaka 21 au atakapooa (akioa kabla ya kufikia umri huu) na akifaa, anawekwa na baraza la ukoo kuwa mlinzi wa watoto wadogo wenzake.

   (25) Watoto wengine wengine vile vile watatoka katika ulinzi wakapofikia umri wa miaka 21 au watakapooa au kuolewa.

   (26) Ikiwa hayupo ndugu yeyote wa ukoo wa watoto, baraza la ukoo wa mama litaweka mlinzi waukoo wake.

   (27) Ikiwa hakuna ndugu kabisa, baraza la hakimu kufuata maombi ya mtu yeyote linaweza kuweka mtu baki kuwa mlinzi wa watoto.

Ulinzi wa mrithi asiyekuwapo:

   (28) Ikiwa mmoja wa warithi hayupo wakati wa kurithi, ndugu mwingine wa ukoo wake huwekwa kuangalia mali mpaka mrithi atakaporudi.

   (29) Mlinzi wa mrithi asiyekuwapo anawekwa na baraza la ukoo, na anapowekwa huelezwa na baraza la ukoo wajibu wake wa ulinzi. Kama hakuelezwa, ni juu yake kupata maelezo ya wajibu wake toka baraza la ukoo.

   (30) Mkubwa kati ya warithi waliopo atafikiriwa kwanza na baraza la ukoo, na ikiwa kwa maoni yao ni mwenye akili ya kutosha na ana tabia nzuri, yeye ndiye atakayewekwa kuwa mlinzi wa mrithi asiyekuwapo.

   (31) Ikiwa warithi wote hawapo baraa la ukoo litaweka mlinzi mmoja wa ukoo ule kuangalia mali yote ya urithi.

   (32) Mlinzi wa marithi asiyekuwapo akipoteza au akiharibu mali ya mrithi anaweza kudaiwa.

   (33) Mlinzi hawezi kuchanganya mali ya urithi pamoja na mali yake: yaani, mali ya mrithi lazima yajulikane wazi.

   (34) Mlinzi hawezi kutumia mwenyewe mali ya mrithi asiyokuwapo.

   (35) Mazao ya mali ya mrithi asiyekuwapo yanaweza kuuzwa kwa shida za nyumbani kwa mrithi: yakiuzwa kwa wingi ni mali ya mrithi.

   (36) Mlinzi wa mrithi asiyekuwapo hapati mashahra wu malipo maalum kwa kazi anayofanya.

   (37) Baraza la ukoo linaweza kumwondoa mlinzi ikiwa hatimizi wajibu wake, na kuweka mwingine, kwa kufuata madai au mashaka ya ndugu yeyote wa mrithi asiyekuwapo.

   (38) Ikiwa hayupo mtu yeyote wa ukoo wa mrithi asiyekuwapo, baraza la hakimu kufuata taarifa ya mtu yeyote linaweza kuweka mtu baki kuwa mlinzi kwa mpango unayofaa.

Ulinzi wa mtu ambaye hawezi kujitegemea:

   (39) Mtu ambaye hawezi kujitegemea kwa sababu ya umaskini au wazimu huwekwa chini ya ulinzi wa mtu wa ukoo wake.

   (40) Mlinzi huyu anawekwa na baraza la ukoo, na wajibu wake ni sawa kama wa mlinzi wa mtoto.

   (41) Kama mtu ambaye hawezi kujitegemea kwea sababu ya umaskini au wazimu huwekwa chini ya ulinzi wa mtu wa ukoo wake.

Ulinzi wa jamaa na mali ya mtu anayesafiri:

   (42) Ikiwa mume anaondoka kwa safari ndefu, anaweza kuchagua mlinzi kuangalia mkewe, watoto na mali yake.

   (43) Mlinzi atasimamia mifugo na kilimo.

   (44) Mlinzi ataangalia mambo yote ya nje yanayohusu nyumba ile, ambayo yangaliangaliwa na mume mwenyewe.

   (45) Mlinzi atashughulika na shida zote za watu wa nyumbani kwa msafiri.

   (46) Mke hawezi kuhama toka mji wa mume wake bila ruhusa ya mlinzi.

   (47) Mke wa msafiri anaweza kufumaniwa na mlinzi.

   (48) Mlinzi anaweza kufungua shauri la ugoni barazani badala ya mume.

   (49) Ni mume tu anayeweza kumwondoa mlinzi.

   (50) Mlinzi aiifa au akihama kabisa na mume hawezi kuarifiwa, baraza la ukoo linaweza kuweka mlinzi mwingine.

   (51) Mlinzi hawezi kudai cho chote kwa kazi yake ya ulinzi.

   (52) Mlinzi akikosa katika wajibu wake wa kuangalia mali ya msafiri na kutunza mkewe na watoto wake, anaweza kuitwa na kuonyea na bareaza la ukoo.

   (53) Akiendelea na makosa yake, mlinzi anaweza kuitwa shaurini na mke au ndugu yeyote wa msafiri katika bareaza la hakimu.

SECOND SCHEDULE
SHERIA ZA URITHI

This section of the article is only available for our subscribers. Please click here to subscribe to a subscription plan to view this part of the article.