SURA YA 2
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, YA MWAKA

YALIYOMO

   Ibara

Kichwa cha Habari

UTANGULIZI

SURA YA KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA

SEHEMU YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU

   1.   Kutangaza Jamhuri ya Muungano.

   2.   Eneo la Jamhuri ya Muungano.

   3.   Tangazo la nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi.

   4.   Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi.

   5.   Haki ya kupiga kura.

SEHEMU YA PILI
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI

   6.   Tafsiri.

   7.   Matumizi ya masharti ya Sehemu ya Pili.

   8.   Serikali na watu.

   9.   Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea.

   10.   [Imefutwa na Sheria Na. 4 ya 1992 ib. 10.]

   11.   Haki ya kufanya kazi, kupata elimu na nyinginezo.

SEHEMU YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU

Haki ya Usawa

   12.   Usawa wa binadamu.

   13.   Usawa mbele ya sheria.

Haki ya Kuishi

   14.   Haki ya kuwa hai.

   15.   Haki ya Uhuru wa mtu binafsi.

   16.   Haki ya faragha na ya usalama wa mtu.

   17.   Uhuru wa mtu kwenda atakako.

Haki ya Uhuru wa Mawazo

   18.   Uhuru wa Maoni.

   19.   Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.

   20.   Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.

   21.   Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.

Haki ya Kufanya Kazi

   22.   Haki ya kufanya kazi.

   23.   Haki ya kupata ujira wa haki.

   24.   Haki ya kumiliki mali.

Wajibu wa Jamii

   25.   Wajibu wa kushiriki kazini.

   26.   Wajibu wa kutii sheria za nchi.

   27.   Kulinda mali ya Umma.

   28.   Ulinzi wa taifa.

Masharti ya Jumla

   29.   Haki na wajibu muhimu.

   30.   Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu.

Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi

   31.   Ukiukaji wa haki na uhuru.

   32.   Madaraka ya kutangaza hali ya hatari.

SURA YA PILI

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA
RAIS

   33.   Rais wa Jamhuri ya Muungano.

   34.   Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.

   35.   Utekelezaji wa shughuli za Serikali.

   36.   Mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu wa kushika nafasi za madaraka.

   37.   Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais, n.k.

   38.   Uchaguzi wa Rais.

   39.   Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais.

   40.   Haki ya kuchaguliwa tena.

   41.   Utaratibu wa uchaguzi wa Rais.

   42.   Wakati na muda wa kushika madaraka ya Rais.

   43.   Masharti ya kazi ya Rais.

   44.   Madaraka ya kutangaza vita.

   45.   Uwezo wa kutoa msamaha.

   46.   Kinga dhidi ya mashtaka na madai.

   46A.   Bunge laweza kumshtaki Rais.

   46B.   Wajibu wa viongozi Wakuu wa vyombo vya Mamlaka ya Utendaji kudumisha Muungano.

SEHEMU YA PILI
MAKAMU WA RAIS

   47.   Makamu mmoja wa Rais, kazi na Mamlaka yake.

   48.   Wakati wa Makamu wa Rais kushika madaraka.

   49.   Kiapo cha Makamu wa Rais.

   50.   Muda wa Makamu wa Rais kushika Madaraka.

SEHEMU YA TATU
WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI

Waziri Mkuu

   51.   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

   52.   Kazi na mamlaka ya Waziri Mkuu.

   53.   Uwajibikaji wa Serikali.

   53A.   Kura ya kutokuwa na imani.

Baraza la Mawaziri na Serikali

   54.   Baraza la Mawaziri.

   55.   Uteuzi wa Mawaziri.

   56.   Kiapo cha Mawaziri na Naibu Mawaziri.

   57.   Wakati na muda wa Mawaziri kushika madaraka.

   58.   Masharti ya kazi ya Mawaziri.

   59.   Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

   60.   Katibu wa Baraza la Mawaziri.

   61.   Wakuu wa Mikoa.

SURA YA TATU

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA
BUNGE

   62.   Bunge.

   63.   Madaraka ya Bunge.

   64.   Madaraka ya kutunga Sheria.

   65.   Muda wa Bunge.

SEHEMU YA PILI
WABUNGE, WILAYA ZA UCHAGUZI NA UCHAGUZI
WA WABUNGE

Wajumbe wa Bunge

   66.   Wabunge.

   67.   Sifa za mtu kuwa Mbunge.

   68.   Kiapo cha Wabunge.

   69.   Tamko rasmi la Wabunge kuhusu maadili ya Viongozi.

   70.   Wabunge kutoa taarifa ya mali.

   71.   Muda wa Wabunge kushika madaraka kama Wabunge.

   72.   Watu wenye madaraka Serikalini kukoma utumishi wanapochaguliwa.

   73.   Masharti ya kazi ya Wabunge.

Tume ya Uchaguzi

   74.   Tume ya Uchaguzi.

Majimbo ya Uchaguzi

   75.   Majimbo ya uchaguzi.

Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge

   76.   Uchaguzi katika Majimbo ya Uchaguzi.

   77.   Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge wa Majimbo ya Uchaguzi.

   78.   Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge Wanawake wa kuchaguliwa na Bunge.

   79.   Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge wa kuchaguliwa na Baraza la Wawakilishi.

   80.   [Imefutwa na Sheria Na. 4 ya 1992 ib. 27.]

   81.   Utaratibu wa kupendekeza majina ya wagombea uchaguzi wa Wabunge Wanawake.

   82.   [Imefutwa na Sheria Na. 4 ya 1992 ib. 29.]

   83.   Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge au sivyo.

SEHEMU YA TATU
UTARATIBU, MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE

Spika na Naibu wa Spika

   84.   Spika na mamlaka yake.

   85.   Naibu wa Spika.

   86.   Utaratibu wa kumchagua Spika na Naibu wa Spika.

Ofisi ya Bunge

   87.   Katibu wa Bunge.

   88.   Sekretarieti ya Bunge.

Utaratibu wa Shughuli Bungeni

   89.   Kanuni za Kudumu za Bunge.

   90.   Kuitishwa kwa mikutano ya Bunge na kuvunjwa kwa Bunge.

   91.   Rais aweza kulihutubia Bunge.

   92.   Mikutano ya Bunge.

   93.   Uongozi wa vikao vya Bunge.

   94.   Kiwango cha vikao vya Bunge.

   95.   Viti vilivyo wazi katika Bunge.

   96.   Kamati za Kudumu za Bunge.

Utaratibu wa Kutunga Sheria

   97.   Namna ya kutumia madaraka ya kutunga Sheria.

   98.   Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii na baadhi ya Sheria.

   99.   Utaratibu wa kutunga Sheria kuhusu mambo ya fedha.

Madaraka na Haki za Bunge

   100.   Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli.

   101.   Kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wa majadiliano na wa shughuli.

SURA YA NNE

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR NA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR

SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA RAIS WA ZANZIBAR

   102.   Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Madaraka yake.

   103.   Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na madaraka yake.

   104.   Uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

SEHEMU YA PILI
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR

   105.   Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Kazi zake.

SEHEMU YA TATU
BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR

   106.   Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na madaraka ya kutunga Sheria za Zanzibar.

   107.   Madaraka ya Baraza la Wawakilishi.

SURA YA TANO

UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO, MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO, TUME YA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA TANZANIA BARA, MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR, MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO NA MAHAKAMA MAALUM YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA
UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

   107A.   Mamlaka ya Utoaji Haki.

   107B.   Uhuru wa Mahakama.

SEHEMU YA PILI
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO

   108.   Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.

   109.   Majaji wa Mahakama Kuu na uteuzi wao.

   110.   Muda wa Majaji wa Mahakama Kuu kushika madaraka.

   111.   Kiapo cha Majaji.

SEHEMU YA TATU
MADARAKA YA KUAJIRI MAHAKIMU NA WATUMISHI WENGINE WA MAHAKAMA ZA TANZANIA BARA NA TUME YA KUAJIRI YA MAHAKAMA

   112.   Tume ya Kuajiri ya Mahakama.

   113.   Madaraka ya kuajiri Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama.

   113A.   Uanachama katika vyama vya siasa.

SEHEMU YA NNE
MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR

   114.   Mahakama Kuu ya Zanzibar.

   115.   Mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.

SEHEMU YA TANO
MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO

   116.   Ufafanuzi.

   117.   Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.

   118.   Majaji wa Mahakama ya Rufani na uteuzi wao.

   119.   Mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.

   120.   Muda wa Majaji wa Mahakama ya Rufani kushika madaraka.

   121.   Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Rufani.

   122.   Kiwango cha vikao vya Mahakama ya Rufani.

   123.   Mashauri yanayoweza kuamuliwa na Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani.

SEHEMU YA SITA
UTARATIBU WA KUPELEKA HATI ZA KUTEKELEZA MAAGIZO YALIYOMO KATIKA HATI ZILIZOTOLEWA NA MAHAKAMA

   124.   Utekelezaji wa maagizo ya Mahakama utafanywa nchini Tanzania kote.

SEHEMU YA SABA
MAHAKAMA MAALUM YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO

   125.   Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

   126.   Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Katiba.

   127.   Muundo wa Mahakama Maalum ya Katiba.

   128.   Utaratibu katika vikao vya Mahakama Maalum ya Katiba.

SURA YA SITA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA NA SEKRATARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

SEHEMU YA KWANZA
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

   129.   Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

   130.   Majukumu ya Tume na taratibu za utekelezaji.

   131.   Mamlaka ya Tume na utaratibu wa shughuli zake.

SEHEMU YA PILI
SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

   132.   Sekretarieti ya Maadili.

SURA YA SABA

MASHARTI KUHUSU MCHANGO WA SERIKALI NA MAMBO MENGINEYO YA FEDHA ZINAZOINGIA KATIKA HAZINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA
MCHANGO NA MGAWANYO WA MAPATO YA JAMHURI YA MUUNGANO

   133.   Akaunti ya Fedha ya Pamoja.

   134.   Tume ya Fedha ya Pamoja.

SEHEMU YA PILI
MFUKO MKUU WA HAZINA NA FEDHA ZA JAMHURI YA MUUNGANO

   135.   Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

   136.   Masharti ya kutoa fedha za matumizi kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

   137.   Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

   138.   Masharti ya kutoza kodi.

   139.   Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya Sheria ya Matumizi kuanza kutumika.

   140.   Mfuko wa Matumizi ya dharura.

   141.   Deni la Taifa.

   142.   Mishahara ya watumishi fulani wa Serikali kudhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

   143.   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

   144.   Kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

SURA YA NANE

MADARAKA YA UMMA

   145.   Serikali za Mitaa.

   146.   Kazi za Serikali za Mitaa.

SURA YA TISA

MAJESHI YA ULINZI

   147.   Marufuku kuunda majeshi ya ulinzi yasiyo majeshi ya Ulinzi ya Umma.

   148.   Madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.

SURA YA KUMI

MENGINEYO

   149.   Maelezo ya mambo yanayohusika na madaraka ya kazi mbalimbali zilizoanzishwa na Katiba hii.

   150.   Maelezo kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka ya kazi katika Utumishi wa Umma.

   151.   Ufafanuzi.

   152.   [Imefutwa na Sura ya 4.]

NYONGEZA YA KWANZA

NYONGEZA YA PILI

ORODHA YA KWANZA

ORODHA YA PILI

SURA YA 2
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, YA MWAKA 1977

[26 April, 1977]

C.A. Acts Nos.
1 of 1977
2 of 1977
Sheria Na.
14 ya 1979
1 ya 1980
28 ya 1980
21 ya 1982
15 ya 1984
14 ya 1990
16 ya 1990
4 ya 1992
20 ya 1992
7 ya 1993
34 ya 1994
12 ya 1995
3 ya 2000
T.S. Na.133 la 2001*

UTANGULIZI
MISINGI YA KATIBA

   KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani: *

   NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo Serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:

   KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.

SURA YA KWANZA (Ib 1-32) Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 5">

JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA

SEHEMU YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU (Ib 1-5)

1.   Kutangaza Jamhuri ya Muungano

   Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

2.   Eneo la Jamhuri ya Muungano Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; Sheria Na. 4 ya 1992 ib. 3">

   (1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

   (2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge; isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika mikoa, wilaya au maeneo mengineyo.

3.   Tangazo la nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 4 ya 1992 ib. 5">

   (1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.

   (2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.

4.   Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.

   (2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.

   (3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano, ambayo ni mambo mengine yote yasiyo Mambo ya Muungano.

   (4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.

5.   Haki ya kupiga kura Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 3 ya 2000 ib. 4">

   (1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.

   (2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo–

   (a)   kuwa na uraia wa nchi nyingine;

   (b)   kuwa na ugonjwa wa akili;

   (c)   kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;

   (d)   kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama mpiga kura,

mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.

   (3) Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo–

   (a)   kuanzisha Daftari la Kudumu la wapiga kura, na kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika Daftari hilo;

   (b)   kutaja sehemu na nyakati za kuandikisha wapiga kura na kupiga kura;

   (c)   utaratibu wa kumwezesha mpiga kura aliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemu nyingine na kutaja masharti ya utekelezaji wa utaratibu huo;

   (d)   kutaja kazi na shughuli za Tume ya Uchaguzi na utaratibu wa kila uchaguzi ambao utaendeshwa chini ya uongozi na usimamizi wa Tume ya Uchaguzi.

SEHEMU YA PILI
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO
WA SHUGHULI ZA SERIKALI (ss 6-11)

6.   Tafsiri Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   Katika Sehemu hii ya Sura hii, isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo, neno "Serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote.

7.   Matumizi ya masharti ya Sehemu ya Pili Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii ya Sura hii.

   (2) Masharti ya Sehemu hii ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya kisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchini haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kama sheria, au hukumu yoyote, inaambatana na masharti ya Sehemu hii ya Sura hii.

8.   Serikali na watu

   (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo–

   (a)   wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;

   (b)   lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;

   (c)   Serikali itawajibika kwa wananchi;

   (d)   wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

   (2) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombo vyake na uendeshaji wa shughuli zake utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.

9.   Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea

   Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha–

   (a)   kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;

   (b)   kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;

   (c)   kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

   (d)   kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;

   (e)   kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;

   (f)   kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;

   (g)   kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;

   (h)   kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;

   (i)   kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;

   (j)   kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;

   (k)   kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.

10.

   [Imefutwa na Sheria Na. 4 ya 1992 ib. 10.]

11.   Haki ya kufanya kazi, kupata elimu na nyinginezo Sheria ya 1984 Na. 15 ib. 6">

   (1) Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi. Na bila ya kuathiri haki hizo, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.

   (2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.

   (3) Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.

SEHEMU YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU (Ib 12-32)

Haki ya Usawa (Ib 12-13)

12.   Usawa wa binadamu Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.

   (2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

13.   Usawa mbele ya sheria Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 8; 3 ya 2000 ib. 5">

   (1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

   (2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

   (3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na Sheria au kwa mujibu wa sheria.

   (4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.

   (5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.

   (6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba–

   (a)   wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika;

   (b)   ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;

   (c)   ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho alipokitenda hakikuwa ni kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;

   (d)   kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;

   (e)   ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.

Haki ya Kuishi (Ib 14-17)

14.   Haki ya kuwa hai Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

15.   Haki ya Uhuru wa mtu binafsi Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru.

   (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo,isipokuwa tu–

   (a)   katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria; au

   (b)   katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.

16.   Haki ya faragha na ya usalama wa mtu Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

   (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.

17.   Uhuru wa mtu kwenda atakako Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.

   (2) Kitendo chochote cha halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya–

   (a)   kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako na kumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au

   (b)   kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda anakotaka ili–

      (i)   kutekeleza hukumu au amri ya mahakama; au

      (ii)   kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na sheria nyingine kuutimiza; au

      (iii)   kulinda manufaa ya umma kwa jumla au kuhifadhi maslahi fulani mahususi au maslahi ya sehemu fulani ya umma, kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara hii.

Haki ya Uhuru wa Mawazo (Ib 18-21)

18.   Uhuru wa Maoni Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa kutoingiliwa kati mawasiliano yake.

   (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

19.   Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 4 ya 1992 ib. 9">

   (1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

   (2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

   (3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.

20.   Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 4; 4 ya 1992 ib. 10">

   (1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

   (2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake–

   (a)   kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya–

      (i)   imani au kundi lolote la dini;

      (ii)   kundi lolote la kikabila pahala watu watokeapo, rangi au jinsia;

      (iii)   eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano;

   (b)   kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano;

   (c)   kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa;

   (d)   kinapigania au kukusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano;

   (e)   hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.

   (3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.

   (4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa yake.

21.   Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 34 ya 1994 ib. 4">

   (1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

   (2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa.

Haki ya Kufanya Kazi (Ib 22-24)

22.   Haki ya kufanya kazi Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila mtu anayo haki ya kufanya kazi.

   (2) Kila raia anastahili fursa na haki sawa, kwa masharti ya usawa, ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyo chini ya Mamlaka ya Nchi.

23.   Haki ya kupata ujira wa haki Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.

   (2) Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki.

24.   Haki ya kumiliki mali Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.

   (2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili.

Wajibu wa Jamii (Ib 25-28)

25.   Wajibu wa kushiriki kazini Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu. Kila mtu anao wajibu wa–

   (a)   kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali na ya uzalishaji mali; na

   (b)   kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia malengo ya uzalishaji ya binafsi na yale ya pamoja yanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria.

   (2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), hakutakuwapo na kazi ya shuruti katika Jamhuri ya Muungano.

   (3) Kwa madhumuni ya ibara hii, na katika Katiba hii kwa jumla, ifahamike kwamba kazi yoyote haita hesabiwa kuwa ni kazi ya shuruti au kazi ya kikatili au ya kutweza endapo kazi hiyo, kwa mujibu wa sheria ni–

   (a)   kazi inayobidi ifanywe kutokana na hukumu au amri ya mahakama;

   (b)   kazi inayobidi ifanywe na askari wa jeshi lolote katika kutekeleza majukumu yao;

   (c)   kazi ambayo mtu yeyote inabidi aifanye kutokana na kuwapo hali ya hatari au baa lolote linalotishia uhai wa ustawi wa jamii;

   (d)   kazi au huduma yoyote ambayo ni sehemu ya–

      (i)   majukumu ya kawaida ya kuhakikisha ustawi wa jamii;

      (ii)   ujenzi wa taifa wa lazima kwa mujibu wa sheria;

      (iii)   jitihada za taifa za kutumia uwezo wa kila mtu kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha jamii na uchumi wa taifa na kuhakikisha maendeleo na tija ya kitaifa.

26.   Wajibu wa kutii sheria za nchi Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.

   (2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.

27.   Kulinda mali ya Umma Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

   (2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.

28.   Ulinzi wa taifa Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.

   (2) Bunge laweza kutunga Sheria zinazofaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi na katika ulinzi wa taifa.

   (3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi, wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa, hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi.

   (4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Masharti ya Jumla (Ib 29-30)

29.   Haki na wajibu muhimu Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilivyofafanulia katika ibara ya 12 hadi ya 28 za Sehemu hii ya Sura hii ya Katiba.

   (2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.

   (3) Raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki, au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake.

   (4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa msingi ya nasaba, jadi au urithi.

   (5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

30.   Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 34 ya 1994 ib. 5">

   (1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

   (2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya–

   (a)   kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;

   (b)   kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya umma;

   (c)   kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai au la jinai;

   (d)   kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au maisha binafsi ya watu wanohusika katika mashauri mahakamani; kuzuia kutoa habari za siri; kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;

   (e)   kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji, uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya watu binafsi nchini; au

   (f)   kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.

   (3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

   (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka sheria kwa ajili ya–

   (a)   kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa mujibu wa ibara hii;

   (b)   kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii.

   (c)   kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii;

   (5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa na hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika, kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe.

Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi (Ib 31-32)

31.   Ukiukaji wa haki na uhuru Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6">

   (1) Mbali na masharti ya ibara ya 30(2), sheria yoyote iliyotungwa na Bunge haitakuwa haramu kwa sababu tu kwamba inawezesha hatua kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa watu wanaoaminika kuwa wanafanya vitendo vinavyohatarisha au kudhuru usalama wa taifa, ambazo zinakiuka masharti ya ibara ya 14 na ya 15 za Katiba hii.

   (2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakati wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa mtu yeyote, isipokuwa tu kwa kiasi ambacho ni lazima na halali kwa ajili ya kushughulikia hali iliyopo wakati wa hali ya hatari au wakati wa hali ya kawaida kushughulikia hali iliyosababishwa na mwenendo wa mtu anayehusika.

   (3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa hai isipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita.

   (4) Kwa madhumuni ya ibara hii na ibara zifuatazo za Sehemu hii "wakati wa hali ya hatari" maana yake ni kipindi chochote ambapo Tangazo la Hali ya Hatari, lililotolewa na Rais kwa kutumia uwezo aliopewa katika ibara ya 32, linatumika.

32.   Madaraka ya kutangaza hali ya hatari Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 4 ya 1992 ib. 11">

   (1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.

   (2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo–

   (a)   Jamhuri ya Muungano iko katika vita; au

   (b)   kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muungano inakaribia kuvamiwa au kuingia katika hali ya vita; au

   (c)   kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii au kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani na usalama; au

   (d)   kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani ya jamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote ambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumia mamlaka ya pekee; au

   (e)   karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au la baa ya kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemu ya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au

   (f)   kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni tishio kwa nchi.

   (3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania Bara nzima au katika Tanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano wa Bunge ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali ya mambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais.

   (4) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti kuhusu nyakati na utaratibu ambao utawawezesha watu fulani wenye kusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemu mahususi za Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumia madaraka aliyopewa na ibara hii kuhusiana na yoyote kati ya sehemu hizi endapo katika sehemu hizi kunatokea yoyote kati ya hali zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na (e) za ibara ndogo ya (2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu hizo; na pia kwa ajili ya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa hali ya hatari.

   (5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibu wa ibara hii litakoma kutumika–

   (a)   iwapo litafutwa na Rais;

   (b)   endapo zitapita siku kumi na nne tangu tangazo lilipotolewa kabla ya kupitishwa azimio lililotajwa katika ibara ndogo ya (3);

   (c)   baada ya kupita muda wa miezi sita tangu tangazo hilo lilipotolewa; isipokuwa kwamba kikao cha Bunge chaweza, kabla ya muda wa miezi sita kupita, kuongeza mara kwa mara muda wa tangazo hilo kutumika kwa vipindi vya miezi mingine sita kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wa kikao hicho wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote;

   (d)   wakati wowote ambapo mkutano wa Bunge utalitangua tangazo hilo kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote.

   (6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au utekelezaji wa masharti ya ibara hii, masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge na ya sheria nyingine yoyote, inayohusu utangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika ibara hii, yatatumika tu katika sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambapo hali hiyo ya hatari imetangazwa.

SURA YA PILI (Ib 33-61)

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA
RAIS (Ib 33-46B)

33.   Rais wa Jamhuri ya Muungano Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 9">

   (1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

   (2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

34.   Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 9; T.S. Na. 133 la 2001">

This section of the article is only available for our subscribers. Please click here to subscribe to a subscription plan to view this part of the article.